Mazungumzo kati ya Iran na IAEA yakamilika bila makubaliano

 


Mazungumzo ya nyuklia kati ya Shirika la kimataifa la kudhibiti nguvu za Atomiki duniani IAEA na Iran kwa mara nyingine yamemalizika bila matokeo madhubuti hapo jana lakini pande zote mbili zimekubaliana kuendelea na mazungumzo. 


Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian na mkuu wa kitengo cha nyuklia nchini humo Mohammad Eslami wamemuhakikishia mkuu wa shirika hilo la IAEA Rafael Grossi kwamba mpango wa nyuklia wa Iran ni wa amani na kwamba taifa hilo halitaki kutengeneza silaha za nyuklia. 


Lakini ombi la Grossi la kufikia maeneo fulani ya vituo vya nyuklia vya Iran kama ilivyoafikiwa kwenye makubaliano ya nyuklia ya mjini Vienna ya mwaka 2015 halikuidhinishwa. 


Baada ya mkutano na Grossi, Amirabdollahian alisema majadiliano kati ya IAEA na Iran yanapaswa kuwa wa kitaalamu na IAEA kama shirika la Umoja wa Mataifa halipaswi kuchukua msimamo wa kisiasa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items