Ticker

6/recent/ticker-posts

Mbinu za kuwa bora katika maisha yako

 

Katika maisha yako unahitaji kutambua mambo mbalimbali yatakayokufanya uweze kuwa bora zaidi, huwezi kusema unataka mafanikio wakati mambo ambayo unajua ni yale mwaka 47. Hivyo kwa kila jambo ambalo unataka kuwa bora katika eneo hilo ni vyema ukajua ni kwa namna gani utaweza kuwa bora. Swali linaweza kunijia ghafla, sasa nafanyaje ili kuwa bora?

Ipo hivi ukitaka kuwa bora katika maisha yako unatakiwa kufanya mambo yafuatayo; 

Kuwa mwaminifu. 
Bila uaminifu katika maisha yako, basi ujue fika mafanikio utayasikia kwa majirani zako waliofanikiwa. Na moja kati ya sabau za kushindwa kufanikiwa katika maisha yetu husasani sisi vijana ni kwamba wengi wetu hatuaminiki.

Wapo baadhi ya watu wakipata kazi huwa wanakuwa wanyenyekevu sana, ila baada siku chache  mara baada ya kuizoea kazi hiyo huwa wanakuwa ni watu ambao hawaminiki hata chembe, roho na hulka zao ni kutaka kufanikiwa kwa haraka, wapo baadhi ya watu hudiriki hata kumuibia mtu ambaye ameawajiri. Kufanya hivyo hufanya mwajiri wake kumfukuza kazi, hata kupelekea doa kwa vijana wengi ya kwamba vijana hatuaminiki.

Hivyo iwe ni mwajiriwa au umejijiri siri kubwa ya kuweza kufanikiwa zaidi ni kuweza  kujijengea misingi  ya uamifu, kwani uaminifu ni siraha iyoisha risasi katika mapambano ya maisha.

Weka vipaumbele.
Maisha bila kuwa na vipaumbele ni sawa yule muhenga aliyesema mtegemea cha nduguye hufa maskini. Mtu ambaye hana viupembele huwa mara nyingi hana muongozo rasmi wa maisha yake na ndio maana hata ukimwambia fanya hiki hata kiwe ni kibaya huwa yupo tayari hii ni kwasababu huwa hana kanuni ambayo inaongoza maisha yake bali huwa yupo tayari kuwasikiliza watu wengine wanasema afanye nini, kwa mantiki hii si sawa hata chembe kama kweli unataka mafanikio ya kweli.

Mara nyingi nimekuwa nikisema hatma ya maisha yako unayo wewe mwenyewe hivyo kila wakati usiwe ni mtu wa kuyumbishwa na jamii ambayo inayokuzunguka, hivyo jifunze kuweka  vipaumbele, hii itakusaidia wewe kwa kiwango kikubwa  kujua ni jambo gani la kufanya na ni lipi si la kufanya.

Kuweka vipaumbele humsaidia mtu katika kiwango kikubwa kuweza kutimiza kusudio lake kwa kiwango kikubwa, endapo utaamua kufanyia kazi vipaumbele hivyo, huwezi kusema unataka kuwa bora harafu vipaumbele ulivyoweka ukawa huviweki katika matendo. Hivyo daima jifunze kujikuweka vipaumbele katika maisha yako.

Sambamba na hilo ili uweze kuwa bora katika maisha yako jifunze kufanya kazi kwa ustadi, na kufanya mambo yale ya msingi. Mara nyingi epuka kufanya kazi zisizo za msingi kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda. Na katika kufanya kazi hizo za msingi ni kwamba lazima uwaze ni kwa jinsi gani kazi hiyo inavyoweza kukupitia kipato.

Ili uweze kuwa bora kila wakati katika maisha yako ipo haja ya wewe  kuweza kuthamini thamani ya muda ulionao katika kufanya kazi. Huwezi kusema unataka mafanikio harafu huwezi kuuheshimu muda ulionao. Muda ulionanao ni mtaji nambari mbili, hii  baada ya kupata mtaji nambari moja, ambao ni mtaji wa uhai. Mtaji muda, wengi wetu tumekuwa tunaupoteza pasipo kujua, hivyo kila wakati ni vyema ukajua thamani ya muda ulionao katika kuyabadilisha maisha yako.

Kwa leo naomba niishie hapa tutakuna siku nyingine ambapo tutazungumza kwa kina  zaidi kuhusu mbinu nyingine ya kuwa bora katika maisha.

Ndimi Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments