Aliyekuwa mshirika wa karibu wa Benjamin Netanyahu ameanza leo kutoa ushahidi dhidi yake katika kesi ya rushwa inayomkabili waziri mkuu huyo wa zamani mjini Jerusalem.
Nir Hefetz, msemaji wa zamani wa Netanyahu, ni shahidi muhimu wa upande wa mashitaka anayetarajiwa kutoa ushahidi muhimu katika kesi hiyo, ambayo inahusu tuhuma kuwa Netanyahu alifanya udanganyifu, akavunja uaminifu na kupokea hongo.
Waziri mkuu huyo wa zamani, ambaye sasa ni kiongozi wa upinzani, anakanusha kufanya kosa lolote. H
efetz aliacha kazi yake ya uandishi wa habari mwaka wa 2009, ili kuwa msemaji wa serikali ya Netanyahu, na katika mwaka wa 2014 akawa msemaji wa familia ya Netanyahu na mshauri.
Baada ya kukamatwa mwaka wa 2018 kuhusiana na kesi ya rushwa ya Netanyahu, Hafetz aliwapa wapelelezi mikanda ya mawasiliano na Netanyahu na familia yake.