Nov 24, 2021

Mzazi, yafahamu mambo muhimu unayopaswa kuwafundisha wanao

  Muungwana Blog       Nov 24, 2021

 

Ikiwa wewe ni mzazni mwema basi unatakiwa kuelewa kwamba kizazi ulichonacho ili kiwe bora basi unatakiwa kuwekeza nguvu na akili nyingi katika kuwafanya wanao waje kuwa ni watu bora zaidi.

Ili uweze kufanya hivyo unatakiwa kuwajenga watoto wako kiakili, hekima busara na maarifa sio kukimbilia kujenga majumba pekee ili waje kuwa warithi wema,usijenge nyumba tu huku wao unawasau ukiamini huo ndio msaada pekee kwa maisha yao ya baadae.

Ukishindwa kuwajenga wao watauza nyumba zote ulizowajengea na kubakia kwenye lindi la umasikini wa kutupwa kwa kuwa hujaweka vitu muhimu vichwani mwao ili kulimda na kuendeleza miradi uliyoacha.

Sijasema uache kujenga nyumba ya kuishi familia ila wale wanaoamini katika ujenzi wa vitu pekee vya ziada na kusahau watu wenye kutumia hayo maendeleo.

Kama hujawaandaa kuyaendeleza watayabomoa na kuanza upya. Hivyo wito wangu kwako ni kwamba kila wakati yakupasa kuwekeza nguvu na akili nyingi katika kuwafundisha wanao, namna sahihi ya kuweza kujitegemea na kuishi katika misingi chanya yenye kuleta mafanikio kwa kiwango cha hali juu.

Pia wafundishe wanao kuweza kuweka bajeti ya kifedha itakayowasaidia wao kwa namna moja ama nyingine kuweza kujikimu hasa pale wanapokuwa wamepatwa na shida mbalimbali.

Yapo mengi ya kuwafundisha wanao, hivyo ni jukumu lako kuanzia sasa kama mzazi kuweza kuwafundisha wanao kuweza kuishi yale yaliyo ya msingi.
logoblog

Thanks for reading Mzazi, yafahamu mambo muhimu unayopaswa kuwafundisha wanao

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment