Ticker

6/recent/ticker-posts

Taliban yaomba EU msaada wa operesheni za viwanja vya ndege


Serikali ya Taliban imeomba msaada wa kuendesha huduma za viwanja vya ndege vya Afghanistan kufuatia mazungumzo ya mwishoni mwa wiki na maafisa wa Umoja wa Ulaya ambayo pia yaliibua wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinaadamu nchini mwao. 


Pande zote ziliwatuma maafisa waandamizi katika mji mkuu wa Qatar, Doha kwa ajili ya mazungumzo hayo, ambayo yalifanyika kabla ya mazungumzo ya wiki mbili kati ya Marekani na Taliban yanayotarajiwa kuanza leo pia mjini Doha. 


Taarifa ya Umoja wa Ulaya imesema mazungumzo hayo hayaashirii kuwa Umoja wa Ulaya unaitambua serikali ya mpito ya Taliban bali ni sehemu ya ushirikiano wa kiutendaji wa Umoja wa Ulaya, kwa ajili ya maslahi ya umoja huo na watu wa Afghanistan. 


Ujumbe wa Taliban uliongozwa na waziri wa mpito wa mambo ya kigeni Amir Khan Mutaqqi wakati upande wa Umoja wa Ulaya uliongozwa na mjumbe maalum wa EU kuhusu Afghanistan Tomas Niklasson.

Post a Comment

0 Comments