Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 26.11.2021

 


Manchester City itapaswa kuongeza juhudi kumpa mkataba wa muda mrefu winga wa England Raheem Sterling, 26 ambaye anahusishwa na Barcelona, ili aweze kusalia klabuni hapo. (Telegraph - subscription required)


Manchester United imeungana na vilabu vingine, vikiwemo Tottenham na Newcastle United, kutaka saini ya mshambuliaji Mserbia Dusan Vlahovic, 21 kutoka Fiorentina. (Mail)


Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Zinedine Zidane wakijiweka sawa na uwezekano wa kocha wao Mauricio Pochettino kuondoka na kujiunga na Manchester United. (Le Parisien, via Metro)


Ralf Rangnick anatarajiwa kuwa kocha wa muda wa Manchester United lakini awali alikataa ofa kutoka klabu hiyo ya Old Trafford kabla ya kukubali masharti mapya ya mkataba huo. (Manchester Evening News)


Manchester United bado inamsaka Pochettino kuchukua mikoba ya umeneja msimu unaokuja, licha ya kuwasili kwa Rangnick. (90 Min)


Kiungo wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 26, anawaniwa na Manchester United kama mbadala wa Paul Pogba, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Old Trafford unakwenda kumaliza mwishoni mwa msimu. (Fichajes - in Spanish)


Barcelona wanafikiria kutupa ndoano kumsajili mshambuliaji wa Basel Arthur Cabral lakini itabidi wauze baadhi ya wachezaji kabla ya kuu kupeleka ofa kwa mbrazil huyo mwenye miaka 23. (Goal)


Mkataba wa winga wa Croatia Ivan Perisic pale Inter Milan unakwisha June 2022 na nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 anasema "chochote kinawezekana, ngoja tuone wiki chache zijazo" alipoulizwa kuhusu mustakabali wake. (Mediaset Infinity, via Football Italia)


Inter Milan wanamatumaini kwamba kiungo wake Mcroatia Marcelo Brozovic,29 atasaini mkataba mpya, mkataba wske wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu. (90 Min) 


Kocha wa AC Milan Stefano Pioli, 56, siku ya Ijumaa atasaini mkataba mpya kuongeza miaka miwili zaidi na kusalia katika klabu hoyo ya Serie A. (Calciomercato, via Football Italia)

Post a Comment

0 Comments