Ukame Somalia waathiri zaidi ya watu milioni 2

 


Umoja wa Mataifa, UN, umesema Ijumaa ukame unaozidi kuwa mbaya nchini Somalia umesababisha zaidi ya watu milioni mbili kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na maji.


UN pia imetahadharisha juu ya msimu wa nne mfululizo wa uhaba wa mvua katika nchi hiyo iliyokumbwa na migogoro.


Ofisi ya kuratibu masuala ya huduma za dharura ya UN (OCHA) imesema takriban watu milioni 2.3 katika wilaya 57 kati ya 74 wamekumbwa na uhaba mkubwa wa maji, chakula na malisho.


Pia imeongeza kuwa visima vya maji vimekauka, na kuongeza hatari ya magonjwa yatokanayo na maji.


Taarifa ya OCHA inaeleza kwamba huu ni msimu wa nne sasa kwa nchi za Pembe ya Afrika kukosa mvua.


Hali mbaya tayari imewalazimu karibu watu 100,000 kukimbia makazi yao kutafuta chakula, maji na malisho ya mifugo yao, shirika la UN lilisema.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi