Shirika la Kazi Duniani la Umoja wa Mataifa, ILO, limesema Ijumaa katika ripoti yake wafanyakazi 50 wahamiaji walifariki nchini Qatar mwaka 2020.
ILO Imeongeza kuwa zaidi ya wafanyakazi 500 walijeruhiwa vibaya, wakati taifa hilo la Ghuba likijiandaa kwa Kombe la Dunia la mwaka 2022.
Ripoti hiyo imetolewa huku kukiwa na ukosoaji zaidi kuhusu mazingira ya kazi kwa maelfu ya vibarua wahamiaji.
Ripoti hiyo pia inawahusisha wale waliojenga viwanja kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Ripoti ya ILO, yenye kichwa cha habari "Moja ni wengi sana", ilisema kuwa sababu kuu ya vifo hivyo ni kuanguka huku ajali nyingi zikitokea mahali pa kazi.