Blinken asema Marekani inaweza kuinufaisha Afrika


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema leo kuwa Marekani inaizingatia Afrika kuwa nguvu kuu ya siasa za kikanda ambapo inaweza kutoa manufaa ya kweli, akitafuta kuimarisha ushawishi wa Marekani wakati China ikiwekeza pakubwa. 


Siku chache kabla ya mpinzani China kuandaa mkutano mkuu kuhusu Afrika nchini Senegal, ambako Blinken ataelekea baadae leo, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani amesema Rais Joe Biden anapanga kuandaa mkutano wa kilele wa viongozi wa Afrika. 


Kwenye hotuba yake katika makao makuu ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi - ECOWAS mjini Abuja, Blinken hakuitaja moja kwa moja China, lakini alisema anafahamu Waafrika wamekuwa na mashaka kuhusu masharti ambayo huambatana na ushirikiano wa kigeni.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi