Makabiliano na Azerbaijan yauwa askari 6 wiki hii: Armenia

 


Armenia imesema leo kuwa wanajeshi wake sita wameuawa katika makabiliano ya mpakani na Azerbaijan karibu na mkoa unaogombaniwa wa Nagorno-Karabakh mapema wiki hii. 


Mapambano hayo ya Jumanne kwenye mpaka wa nchi hizo mbili jirani yalikuwa mabaya zaidi kushuhudiwa tangu zilipoingia vitani mwaka jana kuhusiana umiliki wa Karabakh na kuzusha hofu ya kutokea mmakabiliano mengine katika mzozo wao wa muda mrefu wa mipaka. 


Wizara ya ulinzi ya Armenia ilisema mapema wiki hii kuwa askari wake mmoja aliuawa na wengine 13 kukamatwa na wanajeshi wa Azerbaijan wakati wengine 24 hawajulikani waliko. 


Azerbaijan ilisema mapema wiki hii kuwa saba kati ya wanajeshi wake waliuawa na kumi kujeruhiwa baada ya kuzuka makabiliano yaliyochochewa na Armenia. 


Mpango wa kusitishwa mapigano ulifikiwa Jumanne usiku kufuatia upatanishi wa Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu na unatekelezwa mpaka sasa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi