Wanajeshi wa Sudan wauwawa kwenye mpaka wa Ethiopia

 


Jeshi la Sudan limesema Jumapili kwamba wanajeshi wake 6 wameuwawa wakati wa mapambano kwenye mpaka na Ethiopia.


Tukio hilo limefanyika siku moja baada ya madai kwamba wanajeshi wa Ethiopia pamoja na wapiganaji walifanya mashambulizi kwenye eneo la mpaka ambalo limekuwa likizozaniwa kwa muda mrefu la al Fashaqa.


Ripoti iliyotolewa na chombo cha habari cha serikali mwishoni mwa wiki ilisema kwamba wanajeshi wamepelekwa kwenye eneo hilo ili kuwalinda wakulima wanaovuna vyakula vyao.


Hayo yanajiri wakati Sudan ikikabiliwa na misukosuko baada ya wakuu wa jeshi kuipindua serikali ya mpito ya kiraia mwishoni mwa Oktoba, huku zaidi ya maafisa 100 wakiwa wamekamatwa.


Maandamano makali yalifuatia hatua hiyo na kupelekea kundi hilo kumrejesha tena madarakani waziri mkuu Abdalla Hamdok.Hata hivyo makundi yanayodai demokrasia nchini humo yanaendelea kuushinikiza utawala huo kuwaachilia maafisa waliozuiliwa, pamoja na kuruhusu utawala wa kiraia.

Post a Comment

0 Comments