Dunia yakabiliwa na kitisho kufuatia joto kali kwenye Uzingo wa Arctic


Hii ni rekodi mpya na ya kusikitisha ambayo Shirika la kimataifa la hali ya hewa (WMO) limeweka hivi punde: nyuzi joto 38 liliripotiwa katika jiji la Urusi la Verkhoyansk katika eneo la Arctic mnamo Juni 20, 2020, kiwango kipya cha juu zaidi cha joto ulimwenguni katika eneo la Arctic, hali inaobua kitisho kikubwa cha mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.


Mnamo Juni 2020, kilomita 115 tu kaskazini mwa uzingo wa Arctic, kuliripotiwa digrii 38: Arctic ndio eneo llinalopata joto haraka zaidi ulimwenguni. Verkhoyansk, mji mdogo huko Yakutia na mojawapo ya maeneo yenye baridi zaidi duniani, tangu wakati huo umekuwa na rekodi nyingine ambazo bado hazijathibitishwa. Msimu huu wa joto uliopita kuliripotiwa hali ambayo haijawahi kutokea nchini Urusi.


Viwango vya joto vya mji wa Verkhoyansk vimekuwa vikifuatiliwa tangu mwaka 1885.


Moscow, hata hivyo, imepigia kura ya turufu azimio kuhusu ongezeko la joto duniani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ilikuwa inahusu "kuunganisha hatari za usalama zinazohusiana na hali ya hewa kama nyenzo kuu katika mikakati ya jumla ya kuzuia migogoro".


Hii ni mara ya kwanza kwa WMO kuongeza taarifa za viwango vilivyopindukia vya joto katika eneo la Arctic katika idara yake ya kumbukumbu za hali mbaya ya hewa na ripoti hii imechapishwa wakati kukishuhudiwa wimbi lisilotabirika la viwango vilivyopindukia vya joto kote ulimwenguni.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi