RC Homera apiga ‘stop’ likizo watumishi wa Serikali Mbeya

 


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC), Juma Homera amefuta likizo kwa watumishi wote wa Serikali mkoa huo ambao idara zao zinahusika na ujenzi wa miradi ya miundombinu ya ujenzi wa vyumba  vya madarasa  na madawati ambapo tayari Serikali imetoa fedha za miradi hiyo.


Homera ametoa agizo hilo leo Jumanne Desemba  7, 2021 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mwakibete alipotembelea chanzo cha maji cha Nzovwe kinachosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (Mbeya-Uwwas) huku akibainisha kufuta likizo kwa wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa halmashauri zote, maofisa manunuzi, watendaji wa kata, wahasibu na watendaji wa idara zingine za Serikali.


Amesema kuwa hatoweza kupokea barua za likizo pasipo kupata taarifa za kukamilika kwa ujenzi wa miradi ya madarasa, madawati na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabishara wadogo maarufu kama machinga.


''Hata mimi mwenyewe siwezi kwenda likizo wakati huu ambao Serikalini inaendelea kutoa fedha za miradi sasa nimefuta likizo zote mpaka hapo nitakapojiridhisha miradi hiyo imekamilika kwa wakati ili watoto waingie madarasani kusoma maeneo salama Januari 2022''amesema


Ameongeza kuwa ''Labda mtumishi augue na atakiwe kupelekwa kutibia katika hosptali ya Taifa Muhimbili lakini pia nitaangalia vigezo kama ugonjwa wanaougua utashidwa kutibika katika hosptali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya''amesema.


Post a Comment

0 Comments