Ni miaka 10 tangu kijana mwenye umri wa miaka 27 ambaye hakuwa na uzoefu wa uongozi achukuwe mamlaka. Lakini imekuwaje kuishi chini ya Kim Jong-un?
Sauti ya vilio ilitawala mitaa ya mji mkuu wa Pyongyang.
Wanafunzi wakiwa na sare zao za shule walipiga magoti na kulia kwa masikitiko makubwa. Wanawake walipigwa picha wakishikilia mioyo yao kuoashiri ajinsi walivyopoteza matumaini.
Korea Kaskazini, nchi ambayo inadhibitiwa vikali na chombo cha habari cha kitaifa ilikuwa imetangaza kwamba Kim Jong-il, "kiongozi wao mpendwa", alikuwa amefariki akiwa na umri wa miaka 69. Ilikuwa Disemba 19, 2011.
Kote duniania , wachambuzi wa Korea walikimbilia kwenye madawati yao kutoa faili zao kumhusu mtu mmoja.
Kim Jong-un.
Akiwa na umri wa miaka 27 alitajwa kuwa mrithi mkuu. Lakini ni wachache walifikiri atafanikiwa kwa loloe. Je, jamii inayothamini umri na uzoefu inawezaje kutawaliwa na mtu ambaye hanauzoefu wowote?
Wengi walitabiri mapinduzi ya kijeshi, au unyakuzi wa wasomi wa Korea Kaskazini. Lakini ulimwengu ulimpuuza dikteta huyo mchanga. Kim Jong-un sio tu ameimarisha msimamo wake, ameanzisha enzi mpya inayoitwa "Kim Jong-unism".
Alianza kwa kuwachukulia hatua mahasimu wake na mamia ya watu walinyongwa na baada ya hapo akaelekeza darubini yake kwa kujaribu silaha nne za nyuklia, makombora 100 ya masafa marefu yalirushwa na kuangaziwa kimataifa kwa mazungumzo na rais wa Marekani.
Lakini harakati zake za kutafuta silaha za nyuklia zmekuja na gharama kubwa. Korea Kaskazini sasa iko kwenye mzozo, ni nchi maskini zaidi naimetengwa zaidi kuliko wakati alipochukua mamlakani.
Lakini imekuwaje kuishi chini ya utawala wake?
Waasi kumi wa Korea Kaskazini - akiwemo mmoja wa wanadiplomasia wake wakuu - wanatafakari juu ya miaka 10 ya Kim Jong-un.
Mwanzo mpya
Mwanafunzi Kim Geum-hyok alifanya kitu ambacho kingemfanya apigwe risasi na kuua wa siku ambayo baba yake Kim Jong-un alifariki. Aliandaa sherehe.
"Hiyo ilikuwa hatari sana.Lakini tulikuwa na furha wakati huo," alisema.
Kulingana na yeye, kiongozi huyo mchanga, ambaye anapenda michezo ya kuteleza kwenye barafu na basketball, ilizua hisia ya matarajio ya mawazo mapya na mabadiliko.
"Tulikuwa na matarajio makubwa kwa Kim Jong Un. Alikuwa amesoma nje ya nchi huko Ulaya, kwa hiyo labda angefikiria kwa njia sawa na sisi," alisema.
Geum-hyok alitoka katika familia ya wasomi na wakati huo alikuwa akisoma Beijing, fursa ambayo ni wachache tu wanaopewa nchini Korea Kaskazini.
Maisha ya Uchina yalifungua macho yake kwa ulimwengu uliofanikiwa zaidi na hapo akatafuta mtandaoni ili kupata habari kuhusu nchi yake
"Mwanzoni, sikuamini. Niliamini watu wa Magharibi walikuwa wakidanganya [kuhusu jinsi Korea Kaskazini ilivyokuwa]. Lakini nilikuwa na hisia mseto. Ubongo wangu ulisema huna haja ya kuangalia, lakini moyo wangu ulitaka. kuangalia zaidi."
Watu milioni 25 wa Korea Kaskazini wanadhibitiwa vikali na mara nyingi hawana habari ya kile kinachoendelea duniani au nchini mwao.
Pia wanafundishwa kwamba kiongozi ni mtu mwenye karama ya kipekee na kiumbe ambaye anastahili uaminifu wao wa mwisho.
Kwa Guem-hyok, urithi wa madaraka wa kijana huyu uliwakilisha kitu ambacho hakikuwepo.
Wenye shaka
Lakini wengine walikuwa na mashaka. Katika ukumbi wa mamlaka huko Pyongyang kulikuwa na minong'ono kwamba Kim Jong-un alikuwa mtoto mwenye bahati asiyefaa kutawala.
Ryu Hyun-woo, balozi wa zamani wa Korea Kaskazini nchini Kuwait, aliambia BBC kwamba wenzake walikerwa na uongozi kupitishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mwana.
"Maoni yangu ya kwanza yalikuwa wazo, la mfululizo mwingine?' Wakorea Kaskazini walikuwa wamechoshwa na mfumo huo wa urithi. Hasa miongoni mwa wasomi, tulitaka mambo mapya, 'Kwani hatustahili kuwa na uongozi mpya na tofauti?' Hayo ndiyo mambo tuliyofikiria."
Familia ya Kim imeongoza Korea Kaskazini tangu ilipobuniwa mwaka 1948. Watu wa nchi hiyo wanafundishwa kuwa kizazi cha familia hiyo ni kitakatifu. Ni njia ya kuhalalisha utawala wao.
Ahadi
Katika hotuba yake mwaka 2012, kiongozi huyo mpya aliahidi kwamba Wakorea Kaskazini hawatalazimika "kukaza mikanda tena".
Kwa nchi ambayo ilikuwa imekumbwa na njaa mbaya katika miaka ya 1990 ambayo iliwaangamiza maelfu ya watu, ilionekana kuwa kiongozi wao mpya alitaka kumaliza uhaba wao wa chakula na mateso yao.Lilikuwa tangazo la kutia moyo sana.
Maafisa wa ofisi ya kigeni waliamriwa kuwezesha uwekezaji zaidi wa kimataifa. Na wengine ndani ya nchi waliona mabadiliko pia.
Dereva Yoo Seong-ju kutoka mkoa wa pwani ya mashariki ya nchi anasema alianza kugundua kuwa bidhaa nyingi katika maduka makubwa zilikuwa zimetengenezwa Korea Kaskazini.
Kukabili wapinzani
Azimio la Kim Jong-un la kuwatakia maisha mema watu wake halikuwafikia wale aliowaona kuwa tishio.
Hususan mjomba wake Jang Song-thaek ambaye alikuwa amekusanya mtandao wenye nguvu wa washirika.
Umbali wa mamilioni ya maili kutoka jiji la Pyongyang eneo la kaskazini mwa nchi karibu na mpaka wa China, mwanabiashara Choi Na-rae walikuwa anajiuliza ikiwa Bw Jang anaweza kuwa kiongozi mpya wa nchi.
"Wengi wetu tulikuwa na matumaini kuwa nchi itashirikiana zaidi na China na kwamba tungeweza kuwa huru kusafiri nje ya nchi," alikumbuka.
Kim Jong-un aonya kutokea kwa janga kubwa Korea Kaskazini
"Tulidhani kama Jang Song-thaek angefanikiwa kuchukua madaraka, angeleta mabadiliko mengi ya kiuchumi nchini Korea Kaskazini. Bila shaka hatukuweza kuzungumza hili kwa sauti lakini tulikuwa na matarajio hayo."
Uvumi kama huu ulivunjwa.
Jang Song-thaek alipachikwa jina la "tapeli wa binadamu" na "mbaya zaidi kuliko mbwa" na kisha kunyongwa kwa madai ya kudhoofisha "uongozi wa umoja wa chama".
Kiongozi huyo mchana alikuwa anaonesha ukatili wake.
Kuchukua udhibiti
Makumi ya watu walikimbia kuvuka mpaka hadi Uchina na hatimaye Korea Kusini kuepuka kuchukuliwa hatua na serikali kwa kuonesha wazi uasi wao.
Kim Jong-un aliamua kuzuia visa vya watu kutoroka nchini. Usalama mpakani uliimarishwa vikali.
Ha Jin-woo alifanikiwa kuwasafirisha karibu watu 100 nje ya Korea Kaskazini wakati huo akiwa kama dalali.
"Niliogopa sana nilipoanza lakini nilikuwa na hisia kwamba huu ni wajibu. Tangu nikiwa mdogo nilikuwa na mashaka mengi kuhusu Korea Kaskazini. Kwa nini nimezaliwa hapa kuishi kama mnyama asiye na haki na uhuru? ilibidi nihatarishe maisha yangu kufanya kazi hii."
Lakini hatimaye aligunduliwa na ilizimika kutoroka. Mama yake alikamatwa na kufungwa gerezani ambako alitendewa vitendo vya kikatili vilivyomfanya apooze.
Hili linamuuma sana Jin-wooambaye hata hakumbuki sauti ya mama yake.
0 Comments