Mahakama moja ya Ujerumani leo itaanza kusikiliza kesi inayomkabili daktari mmoja wa Syria anayetuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuwatesa na kuwauwa wafungwa katika gereza la serikali nchini mwake.
Waendesha mashtaka wa serikali ya Ujerumani wanasema daktari huyo aliyetambulishwa kwa jina Alaa M. alifanya kazi katika gereza moja la kijeshi katika mji wa Homs kuanzia Aprili 2011 hadi mwishoni mwa mwaka 2012.
Wanamtuhumu daktari huyo kwa kumuua mtu mmoja, kuwatesa wengine 18 na kusababisha madhara ya kimwili na kisaikolojia kwa mtu mwengine miongoni mwa uhalifu mwengine.
Daktari huyo amekanusha mashtaka hayo. Kesi hii inafuatia hukumu ya wiki iliyopita nchini Ujerumani, iliyotolewa kwa afisa mwandamizi wa zamani katika jeshi la polisi la Syria aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
0 Comments