Marekani: Msomali na Mkenya wanaozuiliwa Guantanamo sasa kuachiliwa


Waafrika wawili ni miongoni mwa wafungwa wa Guantanamo waliotangazwa "kuachiliwa", Jumatano Januari 12, 2022, na Marekani. Wamewekwa kizuizini kwa miaka kumi na tano, bila kufunguliwa mashtaka rasmi. Utawala wa Marekani sasa unaamini kuwa sio tishio tena kwa nchi.


Mohamed Abdul Malik Bajabu ndiye Mkenya pekee aliyezuiliwa Guantanamo. Alikamatwa mwaka wa 2007 na mamlaka ya Nairobi, alikabidhiwa Marekani wiki chache baadaye na tangu wakati huo amezuiliwa kama mfungwa "chini ya sheria ya vita", kauli inayotumiwa na Marekani kwa kumwita watu waliokamatwa kwa madai yenye uhusiano na mapambano dhidi ya ugaidi.


Wakati huo, Mkenya huyo alishutumiwa kuwa na uhusiano wa karibu na al-Qaeda Afrika Mashariki na kushiriki katika mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi mwaka 2012 mjini Mombasa. Miaka kumi na tano baadaye, utawala wa Marekani hatimaye unamwona kuwa "anaweza kuachiliwa" kwa sababu ya "kiwango cha chini cha elimu" na kwa sababu alikuwa katika nafasi ya chini wakati alipokamatwa.


Inabakia kuonekana ikiwa Kenya itakubali makubaliano na Marekani kwa uhamisho wake wa haraka hadi nchini mwake. Vinginevyo, atalazimika kubaki jela hadi Marekani ipate nchi ya tatu ambayo itakuwa tayari kumchukuwa.


Mfungwa mwingine anayehusika ni Guled Hassan Duran. Yeye ni raia wa Somalia, alikamatwa nchini Djibouti mwaka 2004. Kwa mara ya kwanza alikaa siku 900 katika jela za CIA kabla ya kupelekwa Guantanamo. Yeye ndiye mfungwa wa kwanza wa kiwango hiki kutangazwa "kuachiliwa". Lakini hakuna uwezekano wa kuachiliwa hivi karibuni. Marekani hairuhusu uhamisho kwenda Somalia, ambayo inaichukulia kuwa nchi iliyo hatarini

Post a Comment

0 Comments