Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 14.01.2022

 


Manchester United imempa kiungo Mholanzi Donny van de Beek, 24, kwa Newcastle na Borussia Dortmund. (Manchester Evening News)


Manchester United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 25. (La Republica - in Italian)


The Red Devils watatanguliza kumpa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 24, kandarasi mpya msimu huu wa joto. (ESPN)



Klabu hiyo ya Old Trafford inaendelea kuwasiliana na mkufunzi wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino kuhusu nafasi ya meneja. (Le Parisien - in French)


Mshambulizi wa West Ham Jarrod Bowen anataka kuhamia Liverpool, ambao bado wana nia ya kutaka kumnunua Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 25. (Football Insider)


Newcastle wanazidi kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Norwich Muingereza Todd Cantwell, 23. (Rudy Galetti - Calciomercato)


The Magpies wamewasilisha ombi rasmi la kumnunua beki wa Sevilla raia wa Brazil Diego Carlos, 28(Sky Sports)


Newcastle wameambiwa watahitaji kulipa zaidi ya £37m kumsajili beki wa Fiorentina na Serbia Nikola Milenkovic, 24. (Sun)



Tottenham wanatazamia kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, kwa klabu ya Italia, huku Juventus wakiwa na uwezekano mkubwa zaidi. (Mirror)


Southampton wanatarajia kufanya mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa kimataifa wa Albania Armando Broja kutoka Chelsea kuwa wa kudumu. (Sky Sports)


Borussia Dortmund wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25. (Patrick Berger - Sport1)



Jurgen Klopp anatarajia mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi, 26, kusalia Liverpool baada ya dirisha la uhamisho la Januari. (Liverpool FC)


Kuna matumaini yanayoongezeka kwa Liverpool kwamba uhamisho wa majira ya joto wa kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 18, unaweza kufaulu. (Caught Offside)


Arsenal wanaweza kufadhaika katika harakati zao za kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo kwa sababu Juventus hawataki mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aondoke kwa mkataba wa mkopo. (DiMarzio)



Arsenal wana orodha ya wachezaji saba wanaolengwa na wachezaji kama vile Youri Tielemans wa Leicester, 24, Georginio Wijnaldum wa Paris St-Germain, 31, na Bruno Guimaraes wa Lyon, 24. (Mirror)


Aston Villa wameonyesha nia ya kutaka kumnunua mlinda lango wa Paris St-Germain raia wa Uhispania Sergio Rico, 28. (Express)


Villa pia wanajaribu kukamilisha uhamisho wa mlinzi wa Scotland Kerr Smith mwenye umri wa miaka 17 kutoka Dundee United. (Mail)


Watford, Southampton na Norwich wanamfuatilia winga wa Lewes Ollie Tanner mwenye umri wa miaka 19. (Sun)



Meneja wa Leicester Brendan Rodgers anatumai kufanya uhamisho wa mkopo wa winga wa Uingereza Ademola Lookman kutoka RB Leipzig kuwa wa kudumu. (Leicester Mercury)


Burnley wanapambana na Nottingham Forest na Coventry kwa ajili ya mlinzi wa Birmingham na Denmark Kristian Pedersen, 27. (Football Insider)


Manchester City wanavutiwa na kiungo wa kati wa Flamengo raia wa Brazil Matheus Franca,17. . (BolaVip - in Spanish)

Post a Comment

0 Comments