F Vijana 628 wafanikiwa kuhitimu mafunzo ya awali ya JKT, 843 KJ. | Muungwana BLOG

Vijana 628 wafanikiwa kuhitimu mafunzo ya awali ya JKT, 843 KJ.


Na Ahmad Mmow, Nachingwea. 

Jumla ya vijana 628 wamehitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) yaliyodumu kwa majuma 16 katika Kikosi cha Jeshi namba 843 (843 KJ) kilichopo wilayani Nachingwea mkoani Lindi. 


Hayo yalielezwa jana kikosini hapo na kamanda wa  kikosi hicho, Luteni kanali Nyagalu Malecela  wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya vijana hao 628 ambao wamepata  kupitia operesheni Samia Suluhu. 


Kamanda Malecela alisema kikosi hicho kilianza kuwapokea vijana hao wazalendo operesheni Samia Suluhu kujitolea


kutoka  mikoa mbalimbali kuanzia tarehe 5.6.2021. Ikiwa ni operesheni ya tatu ya vijana wa kujitolea katika kikosi hicho. Huku akibainisha kwamba vijana waliopokewa walikuwa 634, wavulana 465 na wasichana 169. 


Alisema vijana hao walianza mafunzo rasmi tarehe 4.10.2021  ambayo yalifunguliwa na yeye kamanda wa kikosi. Hatahivyo hao 628 ndio waliofanikiwa kuhitimu mafunzo hayo. 


 " Vijana sita walishindwa kuendelea namafunzo. Ikiwa ni wavulana watano na msichana mmoja, kutokana na sababu za kiafya na utoro," alisema Kamanda Malecela. 


Kamanda huyo wa 843KJ ambae alibainisha kwamba vijana hao wataendelea kutumikia mkataba wao kwa muda wa miaka miwili ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa  alizitaja changamoto za miundombinu ya barabara na upungufu wa wataalamu wa tiba kikosini kuwa ni miongoni mwa zinazo kabiliwa kikosini hapo. 


" Changamoto zinazo wahusu MMJKT zinaendelea kutatuliwa kwa kadiri ilivyowezekana. Hatahivyo zipo changamoto kadhaa ikiwamo barabara inayotoka kijiji cha Mapochero hadi kikosini ni mbovu,"alifafanua kamanda Malecela. 


Kuhusu upungufu wa wataalamu wa tiba kikosini alisema kumekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ambayo hailingani na idadi ya  wataalamu wanaotoa matibabu kikosini hapo. Hali inayosababisha wagonjwa wengi kukimbiziwa katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea. 


Mgeni rasmi ambae ndiye aliyefunga mafunzo hayo, mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba licha ya kuwaasa vijana hao wakatumikie viapo vyao na mafunzo waliyopata kwa manufaa ya taifa na wenyewe kama lilivyokuwa lengo la kuanzishwa JKT alisema serikali itandelea kushughulikiana kutatua changamoto mbalimbali zilizopo vikosini. Ikiwamo changamoto zilizobainishwa na kamanda huyo wa 843KJ. 


Natayari ipo mipango na mikakati madhubuti ya kutatua changamoto hizo na mawasiliano  ya simu za viganjani haraka. 


Alisema serikali pia inatambua kwamba kuna changamoto ya mawasiliano ya uhakika kupitia simu za kiganjani kikosini hapo. Akaweka wazi kwamba mpango wa kutatua changamoto hiyo utekelezaji wake umefikia hatua kubwa.

Post a Comment

0 Comments