DC Kibaha aamuru Mtendaji wa kijiji kurejesha fedha ya kijiji 650,000

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Sara Msafiri, ameamuru Mtendaji wa Kijiji Cha Ruvu Stesheni Neema Shang’a ambae kwa Sasa kaamishwa kituo Cha kazi kufuatia tuhuma zinazodaiwa kujichotea fedha za Kijiji kinyume na taratibu kiasi cha sh.650,000 azirejeshe Mara moja .

Ameeleza timu ya wakaguzi wa ndani ilifika katika Kijiji hicho miaka miwili kuona matumizi na makusanyo Kama kinafuata taratibu za fedha ambapo ilibaini kutolewa kwa fedha hizo .

Akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Ruvu Stesheni, ambao walifikisha malalamiko kutokuwa na mikutano ya vijiji na mapato na matumizi, Msafiri alieleza wakati jarada linaendelea na uchunguzi  na TAKUKURU kwanza mtendaji huyo anapaswa kurudisha fedha za umma.

Aliwaasa watendaji wengine kuacha kufanya udokozi wa fedha za Kijiji kabla ya vikao vya kupitisha ili fedha itoke kihalali

Mkuu huyo wa wilaya alisema ,hatua hii iwe fundisho kwa wengine ,hata Kama kaamishwa kituo Lakini atume pesa za Kijiji .

“Sheria za fedha zinaelekeza kwamba fedha yoyote ya umma unapoikusanya usiitumie Mpaka upeleke kwenye akaunti ya Kijiji halafu matumizi yake unaandikia hoja unapeleka katika vikao ambavyo vikipitisha ndio ifanyiwe matumizi”

“Kuna fedha zinatolewa zimetumika kinyume na Utaratibu, Sasa ripoti zimekamilika na nimewaagiza wakaguzi wa ndani waje wasome ripoti hiyo ili penye mapungufu na fedha zilizotumika wapewe elimu kamati ya fedha na mipango ili mambo yasijirudie .

Alibainisha ,Kuna watendaji wanaamishwa ambao ripoti ya ukaguzi inaonyesha walifanya matumizi ya fedha kinyume na Utaratibu.

Msafiri aliwaambia mkurugenzi,mwanasheria ,wakuu wa idara ,maofisa utumishi na maofisa ununuzi popote kamati za Serikali za Vijiji zinapotoa hoja ya matumizi ya fedha waende kusaidia Vijijini maana changamoto za miradi ya Ruvu Stesheni zinatokana na mlundikano wa matatizo ambayo Serikali ya Kijiji imefikisha ngazi ya halmashauri Lakini zinacheleweshwa kupatiwa ufumbuzi.

“Na hii inasababisha Mwenyekiti wa Kijiji anaogopa kuitisha mikutano ya wananchi maana anakuwa Hana majibu ya kutoa kwa wananchi.”

Awali baadhi ya wanakijiji walitoa kilio chao juu ya miradi ya maendeleo kukwama ikiwemo Zahanati ya Kijiji kutoanza kazi .

Kutokana na changamoto hiyo Msafiri ,aliitaka Halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,kwa Hali ya jengo ilipofikia kuhakikisha inafanya umaliziaji na kuanza kutoa huduma Juni 25 mwaka huu.

Alitaka ,jengo lianze kutoa huduma za awali za mama mjamzito na watoto wakati wakisubiri vifaa tiba na vyombo vya dola kuendelea na baadhi ya uchunguzi.

 

Post a Comment

0 Comments