Tetesi za soka Ulaya leo 27.05.2022

Manchester United wamemwambia kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, kwamba wataelekeza mawazo yao kwingine kama hatoweza kuamua kama anataka kuja Old Trafford msimu huu wa joto. (Sport)


Pendekezo la kiungo wa Monaco Aurelien Tchouameni kuhamia Real Madrid limezuiliwa kutokana na suala la kodi. Mabingwa hao wa La Liga wako tayari kulipa takriban euro 80m (£68m) kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22. (ESPN)

Manchester United, Liverpool, Arsenal na Chelsea wote wanamtaka Tchouameni na watakuwa tayari kuingilia kati ikiwa uhamisho wake kwenda Madrid hautatimia. (Sun)


AC Milan wanataka kumfunga mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 22, kwenye mkataba mpya wa kukataa nia ya Real Madrid. Wahispania hao wanatafuta mshambuliaji baada ya mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, kuahidi mustakabali wake kwa Paris St-Germain. (La Gazzetta dello Sport)


Mshambulizi wa Everton Richarlison, 25, anaweza kuondoka Goodison Park msimu huu wa joto huku Tottenham, Real Madrid na Paris St-Germain zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Mail)


Everton inashindana na West Ham kumsajili mshambuliaji wa Burnley na Ivory Coast Maxwel Cornet, 25, baada ya Clarets kushushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (Telegraph)


Nahodha wa Tottenham Harry Kane yuko tayari kufanya mazungumzo kuhusu mkataba mpya na klabu hiyo, licha ya mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 kushinikiza kuhamia Manchester City msimu uliopita wa joto. (Evening Standard)


Inter Milan wanatumai kumsajili Henrikh Mkhitaryan, 33, mkataba wake wa sasa na Roma utakapokamilika msimu wa joto. Kiungo huyo wa Armenia pia anafikiria ofa kutoka kwa washindi wa Ligi ya Europa Conference. (Fabrizio Romano)


Arsenal wanavutiwa na kiungo wa Lens Cheick Doucoure, 22. Hata hivyo, Brighton, Everton, Crystal Palace na Wolves pia wanamfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Mali. (Mirror)


Leicester City wanajiandaa kumpa beki wa Ireland Kaskazini Jonny Evans, 34, mkataba mpya wa mwaka mmoja. Hata hivyo, watasikiliza ofa kwa beki wa kati wa Denmark Jannik Vestergaard, 29, na kiungo Mfaransa Boubakary Soumare, 23, huku Brendan Rodgers akijaribu kutikisa kikosi chake. (Mirror)


Manchester United wanaweza kuwasilisha ofa kwa Christopher Nkunku anayelengwa na Liverpool na Chelsea wiki ijayo, huku mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 akisita kusaini mkataba mpya na RB Lepizig. (Florian Pettenberg, Sky Sport)


Paris St-Germain haitamsajili winga wa Barcelona Ousmane Dembele, 25, msimu huu wa joto licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuhusishwa pakubwa na kurejea katika nchi yake. (Le Parisien)


Manchester United pia wamefanya mazungumzo ya ndani na meneja mpya Erik ten Hag kuhusu beki wa Ajax na Uholanzi Jurrien Timber, 20, na beki wa kati wa Villareal kutoka Uhispania Pau Torres, 25. (Caught Offside).


Kinyozi wa Paul Pogba ameacha kidokezo kwenye Instagram kuhusu mustakabali wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, akipendekeza Mfaransa huyo atajiunga tena na Juventus wakati mkataba wake na Manchester United utakapokamilika msimu wa joto. (Manchester Evening News)


West Ham itasikiliza ofa kwa kiungo wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, 27, msimu huu wa joto kufuatia kuripotiwa kutofautiana na meneja David Moyes. (Football Insider)


Fiorentina wanatatizika kukubali dili la kumsajili kiungo wa Arsenal Lucas Torreira. Kiungo huyo wa kati wa Uruguay, 26, alifanya vizuri akiwa na timu ya Italia ambayo inatumai The Gunners itapunguza bei yao ya £12.5m. (Evening Standard)


Uhamisho wa Everton kumnunua mlinda mlango wa Blackpool wa Wales Chris Maxwell, 31, kama msaidizi wa Jordan Pickford, unategemea chaguo lao la tatu, Mreno, Joao Virginia, 22, kukamilisha uhamisho wa kudumu au mkataba mwingine wa mkopo kwa Sporting Lisbon. (Lancashire Live)

 

Post a Comment

0 Comments