Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Trump: Marekani inapaswa kufadhili ujenzi wa shule salama kabla ya msaada kwa Ukraine

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amewataka wabunge wa Marekani kutenga fedha kwa ajili ya usalama wa shule badala ya kutuma msaada wa kijeshi nchini Ukraine.

Akizungumza katika mkutano wa wafuasi wa bunduki, Trump alihoji ni vipi Marekani "ina dola bilioni 40 za kupeleka Ukraine" lakini haiwezi kuhakikisha usalama shuleni.

Mkutano wa National Rifle Association, shirika kubwa zaidi la wamiliki wa bunduki nchini Marekani, unafanyika Houston.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya watu 21 kuuawa kwa kupigwa risasi shuleni Texas.

"Kabla hatujajenga mataifa mengine duniani, tunapaswa kuwajengea watoto wetu shule salama katika taifa letu," Trump alisema katika hotuba ya Ijumaa, huku akishangiliwa sana.

Mapema mwezi huu, Bunge la Marekani lilipiga kura kwa wingi kutuma karibu $40bn (£31bn) kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

Kwa jumla, wabunge wa Marekani wametuma takriban $54bn kwa Ukraine tangu Urusi ilipovamia mwezi Februari.

 

Post a Comment

0 Comments