Tume ya uchaguzi Kenya yamzuia Kalonzo Musyoka kugombea urais

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka hatashiriki kinyang'anyiro cha urais Agosti 9 baada ya tume ya uchaguzi kumfungia.Nation limeripoti

Wakati uo huo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imewaidhinisha wagombea 16 ambao sasa watawasilisha nyaraka zao za uteuzi kuanzia leo.

Orodha hiyo ina wafuasi tisa wa vyama vya siasa/muungano na saba huru.

Wagombea wakuu Raila Odinga (Azimio la Umoja One Kenya Coalition party) na Naibu Rais William Ruto wa United Democratic Alliance ni miongoni mwa walioidhinishwa na IEBC.

Bw Musyoka hakuwasilisha orodha ya wafuasi wake katika karatasi inayohitajika.

Yeye ni miongoni mwa wagombea wanne wa vyama vya kisiasa na wagombea binafsi tisa ambao walishindwa kukidhi matakwa ya IEBC ya wafuasi 48,000 angalau kaunti 24, kuwasilisha ipasavyo majina ya wafuasi na nakala za vitambulisho vyao vya kitaifa.

 

Post a Comment

0 Comments