Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa Ukraine inaweza kutarajia kuhisi matokeo ya vita vya Urusi "kwa miaka 100" kwa sababu ya mabomu ambayo hayakulipuka yanayotapakaa mijini.
"Ndio maana itatubidi pia kufanya kazi pamoja katika ujenzi huo," aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa waandishi wa habari huko Berlin.
Akirejelea historia ya Ujerumani iliyokumbwa na vita, kansela wa Ujerumani alisema "wale wanaoishi Ujerumani wanajua kwamba mabomu kutoka Vita vya Pili vya Dunia bado yanagunduliwa mara kwa mara".
Mnamo Desemba 2020, polisi walifunga barabara na watu walilazimika kuondoka majumbani mwao magharibi mwa Ujerumani kwa sababu bomu la Vita vya Kidunia vya pili lenye uzito wa kilo 500 lilipatikana na ilibidi litatuliwe.
0 Comments