F Waziri Mkuu Majaliwa kufanya ziara mikoa ya Arusha na Tanga leo | Muungwana BLOG

Waziri Mkuu Majaliwa kufanya ziara mikoa ya Arusha na Tanga leo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 23, 2022 anafanya ziara ya siku moja katika mkoa wa Arusha na Tanga ambapo atashuhudia zoezi la awamu ya Pili ya wananchi takribani 117 kutoka kaya 27 wanaohama kwa hiari yao wenyewe kutoka katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kijiji cha Msomera, Handeni

Mheshimiwa Majaliwa pia atakagua Makazi na miundombinu ya huduma kwa wananchi katika kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga

Pia Mheshimiwa Majaliwa atakagua alama zilizowekwa kubainisha eneo la hifadhi ya pori tengefu la Loliondo la Kilometa za mraba 1500.

Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza wakazi hao kwa maamuzi yao ya kuhamia Katika kijiji cha Msomera ambapo amewahakikishia kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ipo pamoja nao.

 

Post a Comment

0 Comments