Wakala wa Frenkie de Jong ameiambia Manchester United kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 25, yuko tayari kuondoka Barcelona lakini hataki kuhamia Old Trafford. (Sport - In Spanish)
Barcelona wamemwambia De Jong kuwa wanataka aondoke katika klabu hiyo na kujiunga na Manchester United. (The Athletic)
Barca wanafikiria kumuacha De Jong nje ya kikosi kwenye ziara yao ya Marekani kwa nia ya kumfanya akubali kuhamia Red Devils. (Sport - In Spanish)
Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo anatazamiwa kukataa ofa nono ya kujiunga na klabu moja ya Saudi Arabia, huku Bayern Munich na Atletico Madrid zikimhitaji mshambuliaji huyo wa Ureno, 37. (ESPN)
Juventus wamewasiliana na Arsenal kuhusu kumsajili mlinzi wa Brazil Gabriel Magalhaes, 24, kuchukua nafasi ya mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, ambaye anatarajiwa kujiunga na Bayern Munich. (Independent)
Mlinzi wa kulia wa wachezaji wa chini ya miaka 21 wa England Djed Spence, 21, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa muda mrefu kutoka Middlesbrough hadi Tottenham Hotspur na ada ya takriban £12m ikiwa imekubaliwa. (Times)
Barcelona wamehusishwa na kutaka kumnunua kiungo wa kati wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 19 Carney Chukwuemeka, 18, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa Aston Villa. (Mundo Deportivo)
Arsenal wanashughulikia mpango wa kumsaini beki wa kushoto wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 25, kutoka Manchester City. (Athletic)
Arsenal pia inatafuta chaguo la kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania Sergio Gomez, 21, kutoka Anderlecht.
Ikiwa watamleta Zinchenko au Gomez basi Nuno Tavares anaweza kuondoka, huku Marseille ikimtaka mlinzi huyo wa kushoto wa Ureno mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano, Twitter)
Arsenal wanashughulikia mpango wa kumsaini beki wa kushoto wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 25, kutoka Manchester City. (Athletic)
Arsenal pia inatafuta chaguo la kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania Sergio Gomez, 21, kutoka Anderlecht.
Ikiwa watamleta Zinchenko au Gomez basi Nuno Tavares anaweza kuondoka, huku Marseille ikimtaka mlinzi huyo wa kushoto wa Ureno mwenye umri wa miaka 22. (Fabrizio Romano, Twitter)
Leeds United wanakaribia kuafikiana kuhusu mkataba wa euro 25m (£21m) na Paris St-Germain ili kumsajili mshambuliaji Mfaransa Arnaud Kalimuendo, 20. (90min).
Beki wa Everton Muingereza Jarrad Branthwaite, 20, atajiunga na PSV Eindhoven kwa mkopo wa msimu mzima. (Guardian)
Ajax wametoa ofa kwa mlinzi wa Rangers wa Nigeria Calvin Bassey, 22, huku klabu za Ligi ya Premia zikiwemo Brighton zikiwa na nia ya kutaka kumnunua. (Mail)
Mazungumzo yanaendelea kati ya Arsenal na wawakilishi wa kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Youri Tielemans, 25. (Football London)
Arsenal pia wanavutiwa na Lucas Paqueta wa Lyon, lakini bado hawajawasilisha ofa kwa kiungo huyo wa kati wa Brazil, 24. (Media Foot - in French)
Everton wanasalia kwenye mazungumzo na Wolves kuhusu kumsajili kiungo wa kati Muingereza Morgan Gibbs-White, 22, baada ya dau la pauni milioni 25 kukataliwa wiki iliyopita. (Sky Sports)
Newcastle United wanaangalia malengo tofauti baada ya kukata tamaa kumsajili mshambuliaji wa Real Sociedad na Sweden Alexander Isak, 22, na winga wa Ufaransa Moussa Diaby, 23, kutoka Bayer Leverkusen, kwa sababu ya ada na mahitaji ya mishahara. (Telegraph)
Winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane, 26, ametolewa ofa kwa Real Madrid. (Marca)
Paris St-Germain wanavutiwa na mshambuliaji wa Benfica Mreno Goncalo Ramos, 21, na mshambuliaji wa Reims Mfaransa Hugo Ekitike, 20. (Fabrizio Romano, Twitter)
PSG pia wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Khephren Thuram, 21, mtoto wa gwiji wa Ufaransa Lilian Thuram, kutoka Nice. (L'Equipe)
West Ham wametoa ofa ya pauni milioni 33.9 kwa Sassuolo euro 40m kwa ajili ya mshambuliaji wa Italia Gianluca Scamacca, 23, wakati PSG wametoa ofa ya euro 35m (£29.7m). (Fabrizio Romano, Twitter)
AC Milan wanajiandaa kumpa winga wa Ureno Rafael Leao kandarasi mpya ya muda mrefu kwani wanasita kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa Chelsea kwa bei ya chini ya pauni milioni 127. (Mail)
Kiungo wa kati wa zamani wa Uhispania Cesc Fabregas, 35, anatazamiwa kusajiliwa na klabu ya Serie B ya Italia Como baada ya kuondoka Monaco. (Gianluca di Marzio)
Southampton na Leicester wanavutiwa na mlinzi wa kati wa Uingereza Levi Colwill, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Huddersfield. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 hajaomba uhamisho wa kudumu kutoka Chelsea lakini anatafuta ufafanuzi kuhusu mustakabali wake wa muda mrefu. (CBS Sports, Twitter)
Mazungumzo yanaendelea kati ya Nottingham Forest na Huddersfield kuhusu kiungo Lewis O'Brien, 23, na beki wa kushoto Harry Toffolo, 26, huku Forest aliyepandishwa daraja akiwa amewasilisha ombi kwa wachezaji wawili wa Uingereza. (Football Insider)
Beki wa kati wa Marekani, Auston Trusty anakaribia kuhamia Birmingham City kwa mkopo atakapotua Arsenal.
The Gunners walimsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari lakini akabaki na Colorado Rapids kwa mkopo hadi msimu huu wa joto. (Dakika 90)
0 Comments