Mjane wa Kobe Bryant amelipwa fidia ya $16m (£13.6m) kama kutokana na kuvuja kwa picha za ajali ya helikopta iliyoua nyota huyo wa mpira wa kikapu wa Marekani na bintiye mwaka wa 2020.
Vanessa Bryant, 40, alisema alipatwa na hofu baada ya kubaini picha zilizopigwa na polisi wa Kaunti ya Los Angeles na maafisa wa zima moto zimesambazwa.
Mahakama ilisema kuwa kaunti lazima imlipe Bi Bryant kwa usumbufu iliyompatia.
Mshtaki mwenza Christopher Chester atalipwa $15m. Mume wa Bi Bryant Kobe Bryant, 41, binti Gianna, 13, na marafiki sita wa familia walikufa wakati helikopta yao ilipoanguka California mnamo Januari 2020.
Bw Chester alipoteza mkewe Sarah na binti Payton katika ajali hiyo.
Ripoti ya Los Angeles Times inayodai wafanyakazi wa kaunti walipiga picha kwenye eneo la ajali na kuwasambazi picha watu wengine imewakasirisha wanafamilia wa waathiriwa.
0 Comments