https://monetag.com/?ref_id=TTIb Jumuiya ya Afrika Magharibi imewekea vikwazo kwa serikali ya Guinea | Muungwana BLOG

Jumuiya ya Afrika Magharibi imewekea vikwazo kwa serikali ya Guinea

 


Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) imeamua kuwawekea vikwazo watu binafsi katika serikali ya kijeshi ya Guinea ili kukabiliana na mapinduzi ya mwaka jana mjini Conakry.


Viongozi hao kutoka umoja huo walikutana mjini New York walikokuwa wakihudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.


Walikubaliana juu ya ‘’vikwazo vya taratibu’’ kwenye orodha ya watu wanaohusishwa na serikali ya Guinea ambao watatambuliwa ‘’hivi karibuni,’’ shirika la habari la AFP linaripoti.


Viongozi wa Guinea wanasema wanahitaji miaka mitatu kuirejesha nchi hiyo katika demokrasia na hawajafurahishwa na matakwa ya Ecowas ya kutaka mabadiliko ya haraka katika kipindi cha mpito.


Katika taarifa yake, waziri mkuu wa mpito wa Guinea, Bernard Gomou, awali alimuelezea mkuu wa Ecowas na rais wa nchi jirani ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, kama ‘’kibaraka’’ na mtu ‘’aliyefurahi kupita kiasi’’ ambaye ‘’alilazimisha kuingia’’ kuongoza shirika la kikanda.


Guinea ilisimamishwa kuwa miongoni mwa nchi za Ecowas kufuatia mapinduzi ya Septemba mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments