Kimbunga Ian chachelewesha jaribio la roketi ya Nasa kwenda mwezini

 


Uzinduzi wa roketi yenye nguvu zaidi kuwahi kutokea katika NASA umecheleweshwa kutokana na dhoruba ya kitropiki ambayo inaweza kuwa kimbunga.


Roketi ya Artemis I Moon ilitarajiwa kurushwa kutoka Kituo cha anga cha Kennedy, huko Florida, Jumanne.


Lakini jimbo la Marekani linakabiliwa na tishio la kimbunga huku dhoruba ya kimbunga Ian ikiimarika na inaweza kukaribia Florida mapema wiki ijayo kama kimbunga kikubwa.


Uzinduzi wa roketi hiyo tayari ulikuwa umeahirishwa mara mbili.


Chombo cha mfumo wa Anga (SLS) limeundwa ili kuwatuma wanaanga na vifaa vyao kurudi Mwezini baada ya kukosekana kwa miaka 50.


Jaribio lake la kwanza halikufaulu mwishoni mwa Agosti kutokana na hitilafu za kiufundi, wakati jaribio la pili mwanzoni mwa Septemba lilitatizwa na kuvuja kwa mafuta.


Uamuzi wa iwapo roketi hiyo itarejeshwa kwenye eneo lilipoundwa unastahili kuchukuliwa na timu ya Artemis I siku ya Jumapili.


Hatua hii itakuwa "kuruhusu ukusanyaji wa data zaidi na uchambuzi," NASA ilisema.

Post a Comment

0 Comments