Na Timothy Itembe Mara.
Maofisa wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Sirari wilayani Tarime mkoani Mara jana kwa kushirikiana na jamii wamekamata shehena ya mafuta ya ingene ya magari makubwa.
Akizungumzia kukamatwa kwa mafuta meneja mkoa Mara,Adam Ntoga alisema tumekamata mafuta bya Ingene ya magari makubwa aina ya na kuwa kumatwa bidhaa hiyo ya magendo imetikana na ushirikiano mwema wa TRA pamoja na jamii inayowazunguka kutoa taarifa.
"Tumefanikiwa kukamata shehena ya mafuta CALTEX DELO GOLD ULTRA SEA W-40 MULTGRADE ya Ingene za magari makubwa katoni 53 zenye jumla ya ujazo wa lita 972 ya kutoka nchi jirani ya Kenya kufanikiwa kumakatwa ni kutokana na wasamaria wema kutoa taarifa akiwemo mwenyekiti wa mtaa huo jina tumelihifadhi"alisema Meneja huyo.
Afisa huyo aliongeza kuwa baada ya kukamatwa kwa bidhaa hiyo kwa ushirikiano wa mwenyekiti wa mtaa akishuhudia mwenyekiti wa mtaa huo ambapo walikamata bidhaa zikiwa zimetunzwa ndani ya nyumba ya Bhoke Mwita Marwa ambayer baadaye alijisalimisha kituo cha mamlaka ya mapato Sirari ambapo alisema hatua zaidi zitafuata ili kujua kama atalipa faini itakayokuwa inamkabili kuilipa.
Ilidaiwa kuwa magendo hayo ya mafuta yalipita mpakani mwa Kenya na Tanzania kwa njia za panya ambapo boda boda walisomba kwa kutumioa usafiri wa pikipiki 3 ambazo bado zinasakwa na zikikamatwa sheria itachukua mkondo wake.
Wafanyabiashara na watoa huduma wametakiwa kufanyashuguli kwa kuzingatia sheria za kodi zilizopitishwa na wawakilishi ambao ni wabunge wa jamuhuri kwa ajili ya usitawi wa Taifa kwa mjibi wa sheria ya kodi.
Sheria hiyo inabainisha kuwa mfanyabiashara ama mtoa huduma ambaye atabainika kuwepa kodi akikamatwa atalazimika kulipa asilimia 100 ya kodi aliyotakiwa kulipa kama adhabu,kwamba kodi hiyo itakuwa mara mbili ya kodi anayodaiwa mteja ambapo mapendekezo ya kuweka kwa adhabu hiyo yamefanywa na Wabunge wa Jamuhuri.
Kwa maana hiyo ayakayebainika akikwepa kodi itakuwa imezidishwa mara mbili ya iliyotakiwa kutozwa kama mtu huyo atakuwa amekwepa.
Meneja huyo alibainisha kuwa bidhaa hiyo iliyokamatwa inaitia hasara serikali zaidi ya shilingi milioni kumi na saba na kuonya kuwa watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo kwa nchi yao ili kujali kulipa kodi kwa maendeleo na ustawi wa Taifa.
Afisa huyo wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Sirari aliosema na kutaja mhusika kuwa walifanikiwa kukamata shehena ya mafuta ya ingene zamagari makubwa yakiwa yamefichwa ndani ya nyumba ya Bhoke Mwita Marwa mkazi wa mtaa wa Mogabiri kata ya Kitare Halmashauri ya mji Tarime.
Kwa upande wa Boneventure Chinguwile mmoja wa maafisa wa TRA Sirari alisema kukamatwa kwa shehena hiyo kumekuja baada ya Waziri wa fedha na mipango Mwigulu Ncxhemba kuja na kufanya mkutano mpakani hapo na kuonya tabia ya kufanya magendo.
0 Comments