Hotuba za viongozi wa dunia zinaendelea kutolewa katika hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa katika makao makuu ya umoja huo mjini New York.
Katika hotuba yake ya kwanza mbele ya hadhara hiyo kama rais wa Iran, Ebrahim Raisi amesema Marekani ''imekanyaga'' makubaliano juu ya mpango wa kimataifa juu ya nyuklia ya Iran uliosainiwa mwaka 2015, na kuongeza kuwa Iran haina nia ya kuunda silaha za atomiki.
Kiongozi huyo pia amesema kuwa Iran inayo nia ya kuwa na uhusiano mwema na majirani zake wote. Aidha, Raisi amepinga vikali vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za magharibi dhidi ya nchi yake, akivitaja kuwa adhabu ya jumla kwa watu wa Iran.
Baadaye Leo, rais wa Marekani Joe Biden atatoa hotuba yake, akitarajia kuishambulia vikali Urusi kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine, na kuhamasisha uungwaji mkono wa mataifa mengine kuisaidia Ukraine kujilinda.
0 Comments