Urusi yasema haikuwa na chaguo ila kuchukuwa hatua za kijeshi Ukraine


Urusi jana ilijieleza kuhusu vita vyake nchini Ukraine na kurudia malalamiko yake kuhusu taifa hilo jirani na mataifa ya Magharibi na kuliambia baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwamba haikuwa na chaguo zaidi ya hatua za kijeshi. 


Baada ya siku za kadhaa za hatua hiyo ya Urusi kukosolewa, katika kongamanano hilo mashuhuri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alibadili mwelekeo kwa kuigeukia Marekani.


Hotuba yake ilijikita katika madai kwamba Marekani na washirika wake, zinahujumu kwa nguvu mfumo wa kimataifa ambao Umoja wa Mataifa unawakilisha na sio Urusi kama nchi za Magharibi zinavyosisitiza. 


Lavrov anayashtumu mataifa ya Magharibi kwa kulenga kuharibu na kuigawanya Urusi ili kuiondoa katika ramani ya kisiasa ulimwenguni, eneo ambalo ambalo limekuwa huru mno.

Post a Comment

0 Comments