Ticker

6/recent/ticker-posts

Wakulima Morogoro wahofia upungufu wa chakula


Wakulima na wadau wa kilimo mkoani Morogoro, wameiomba serikali kuangalia upya suala la kufungua mipaka ya nchi, jambo ambalo limepelekea wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kuingia nchini na kununua mazao yakiwa mashambani na mashineni licha ya kuwepo na mavuno machache msimu uliopita.


Hali hiyo imetajwa kusababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei za mazao ya nafaka ikiwemo mahindi, mchele pamoja na mazao mengine hapa nchini kutokana na kuwepo kwa upungufu wa mazao hayo.


Wakizungumzia hali hiyo mkoani humo  ambayo kwa sasa wanadai imepelekea mazao ya chakula kupanda serikali ina kila sababu za kuingilia kati ili kunufaisha wafanyabiashara wa ndani.


Kwa upande wao baadhi ya wadau wa kilimo mkoani Morogoro, wameeleza athari za kupanda kwa bei za mazao na kuishauri serikali kuhusu kufunguliwa kwa mipaka ambayo imepelekea wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kuja Tanzania kuchukua mazao ya chakula.

Post a Comment

0 Comments