F Rc Babu Aanza Harakati Za Mji Wa Moshi Kuwa Safi,atoa Maagizo Ya Watu Kuchukuliwa Hatua | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Rc Babu Aanza Harakati Za Mji Wa Moshi Kuwa Safi,atoa Maagizo Ya Watu Kuchukuliwa Hatua



Mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro umeanza tena jitihada za kuimarisha usafi na  kuendelea kushika nafasi yake ya kwanza katika Mashindano ya Usafi wa Mazingira yanayofanyika kila mwaka kwa uratibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii huku uki hakikisha utekelezwaji wa sheria ndogo ya usafi na Mazingira ya mwaka 2006 na Marekebisho yake ya mwaka 2019 inafuatwa.


Utaratibu huo wa kuanza usafi umezinduliwa leo Oktoba 8.2022 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu ambapo ametangaza kuwa zoezi la kufanya usafi litakuwa kila siku ya Jumamosi ndani ya Manispaa ya Moshi ambapo wafanyabiashara na wananchi watakao chafua mazingira watachukuliwa hatua kali za kisheria.


"Tumezindua rasmi zoezi la kufanya usafi kila siku ya Jumamosi,hili ni agizo tunataka kurudisha Mji wa Moshi katika heshima yake ya kuongoza kwa usafi kila tunapo tathiminiwa na kukaguliwa,ni wajibu wa kila mmoja kushiriki zoezi hili kikamilifu"alisema Baba


Mhe.Babu ameongeza kuwa zoezi hilo la kufanya usafi litakuwa kila wiki siju ya Jumamosi na watakao kaidi watachukuliwa hatua.


"Kila siku ya Jumamosi zoezi la usafi litakuwa likifanyika kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu kamili asubuhi,serikali haitaki kugombana na mtu,nitakuwa napita mwenyewe kukagua hali ya usafi katika maeneo yetu vilevile na Jumamosi ya mwisho wa mwezi watakao kaidi watachukuliwa hatua " alisema Babu


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soko la Mbuyuni Lameck Mziray ambapo zoezi hilo la usafi lilizinduliwa,amepongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa na watendaji wake kuona umuhimu wa kurudisha heshima ya usafi wa mji wa Moshi.


"Nikazi nzuri imefanyika ila naona itakuwa kwa muda mfupi sana maana hata ile Jumamosi ya mwisho wa mwezi wananchi hawajitokezi sasa ikiwa Mkuu wa Mkoa ameahidi kisimamia hili,watakao chafua mazingira na wafanyabiashara wasio fanya usafi wachukuliwe hatua za kisheria na siyo lelemama" alisema Mziray


Kwa upande wao Wananchi walio shiriki zoezi hilo Mwajuma Mdee na Joshu Mathew wameeleza kuwa uchafu mwingi umekuwa ukitupwa na walinzi wa usiku na Mama Ntilie hivyo wadhibitiwe haraka ili zoezi la usafi lifanikiwe.


Hadi kufikia mwezi Agosti, mwaka huu, takwimu zinaonesha kuwa mji wa Moshi unazalisha jumla ya tani 236 za taka  kila siku yakiwemo mabaki ya mboga mboga na matunda ambayo ni mali ghafi ya Kiwanda cha mboji na uzalishaji huo ni sehemu ya kuufanya mji wa Moshi kuwa safi.

Post a Comment

0 Comments