https://monetag.com/?ref_id=TTIb Jeshi la Rwanda lamuua mwanajeshi wa Kongo aliyevuka mpaka | Muungwana BLOG

Jeshi la Rwanda lamuua mwanajeshi wa Kongo aliyevuka mpaka




Wanajeshi wa Rwanda wamemuua kwa kumpiga risasi mwanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye alivuka mpaka kati ya nchi hizo mbili hapo jana. Taarifa hii imethibitishwa na wizara ya ulinzi ya Rwanda na jeshi la Kongo. 


Mamlaka za Rwanda zimesema mwanajeshi huyo aliwasili katika eneo la Rubavu na kuanza kuwafyatulia risasi maafisa wa jeshi la ulinzi. Msemaji wa jeshi la Kongo, Kanali Guillaume Ndjike amesema askari huyo alijiunga na jeshi hivi karibuni na huenda alipotea katika eneo hilo la mpakani wakati wa doria ya usiku huku akisema kuwa uchunguzi unaendelea. 


Mvutano umekuwa ukiongezeka kati ya Kongo na Rwanda. Siku ya Ijumaa rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana juu ya umuhimu wa waasi wa M23 kusitisha mapigano na kujiondoa katika maeneo wanayoyadhibiti mashariki mwa Kongo.

Post a Comment

0 Comments