Mazungumzo hayo yaliyopatanishwa na viongozi wa kanda yaliangazia kuzorota hali ya usalama na tishio linaloletwa na waasi wa M23 juu ya uthabiti wa eneo la maziwa makuu. Mkutano huo uliunga mkono kuendelea kutumwa kwa wanajeshi chini ya jeshi la kikanda na kuharakisha juhudi za kupokonya silaha vikundi vya wanamgambo.
Viongozi kutoka DRC na Rwanda walikutana kwa mara ya kwanza kufuatia mzozo wa kidiplomasia uliosababishwa na mgogoro unaoendelea katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.
Mkutano huo wa kilele ulioongozwa na Rais wa Angola Joao Laurenco uliunda ratiba ambayo inatanguliza hatua muhimu ikiwa ni pamoja na kukomesha uhasama, kuwaondoa waasi wa M23 kutoka katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kurejea katika nafasi zao za awali.
Waliidhinisha uingiliaji kati wa kijeshi dhidi ya kundi hilo iwapo watashindwa kutii.
Wakuu hao wa nchi walielezea wasiwasi wao juu ya ukosefu wa usalama ulioenea na mashambulizi ya kudumu ya kundi la M23 dhidi ya jeshi la Kongo. Walikubaliana kwamba makundi yote yenye silaha yanayoendesha shughuli katika eneo la Kongo yanapaswa kuweka chini silaha zao.
0 Comments