Chama cha upinzani cha Kuomintang (KMT) kilishinda maendeo kadhaa muhimu siku ya Jumamosi, yakiwemo ya mji mkuu Taipei.
Kura hiyo imevuta hisia za kimataifa huku Taiwan ikizidi kuwa kitovu kikubwa cha siasa za kijiografia kati ya China na Marekani.
"Matokeo ya uchaguzi hayakuwa yalivyotarajiwa...ninafaa kubeba jukumu lote na nijiuzulu kama mwenyekiti wa DPP mara moja," Bi Tsai, ambaye ataendelea kuwa rais wa kisiwa hicho kinachojitawala, aliwaambia wanahabari.
Uchaguzi wa mabaraza ya mitaa na mameya wa jiji kinadharia unazingatia masuala ya ndani, inayoshughulikia masuala kama vile uhalifu, makazi na ustawi wa jamii, na wale waliochaguliwa hawatakuwa na sauti ya moja kwa moja kuhusu sera ya Taiwan kuhusu China.
Hata hivyo, Bi Tsai na maafisa wa serikali waliwataka wapiga kura kutumia uchaguzi huo kutuma ujumbe kuhusu kusimama kwa demokrasia, huku Beijing ikiongeza shinikizo katika kisiwa hicho.
0 Comments