Kundi hilo lilikuwa na hatia ya "uhalifu wa kimaadili" ikiwa ni pamoja na uzinzi, wizi na mapenzi ya jinsia moja, afisa wa Taliban aliambia BBC.
Hii inadhaniwa kuwa ni mara ya pili ndani ya mwezi mmoja kundi hilo la Kiislamu kufanya adhabu ya viboko hadharani.
Hatua hiyo inaweza kuashiria kurejea kwa itikadi kali zilizoonekana katika utawala wa awali wa Taliban katika miaka ya 1990.
Omar Mansoor Mujahid, msemaji wa Taliban wa eneo la Logar mashariki mwa Afghanistan, ambapo shambulio hilo lilitokea, alisema kuwa wanawake wote watatu waliachiliwa baada ya kuadhibiwa.
Baadhi ya wanaume hao walifungwa jela, alisema, lakini haijulikani ni wangapi.
Wanaume na wanawake hao walichapwa viboko kati ya 21 na 39 kila mmoja. Idadi ya juu ambayo mtu anaweza kupokea ni 39, afisa mwingine wa Taliban alisema.
Watu 19 pia waliadhibiwa wiki iliyopita katika kuchapwa viboko sawa na hivyo katika jimbo la Takhar kaskazini mwa Afghanistan, ripoti zinasema.
0 Comments