Waziri Mkuu wa zamani wwa Pakistan, Imran Khan, amenusurika kifo baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bunduki alipokuwa akifanya maandamano katika mji wa Wazirabad mashariki mwa nchi.
Alijeruhiwa mguuni na watu wengine wanne pia walijeruhiwa baada ya jukwaa lao-kontena lililokokotwa na lori kushambuliwa kwa risasi.
Hakuna kauli yoyote rasmi iliyotolewa kuhusu nia ya shambulio hilo ambalo washirika wanasema lilikuwa ni jaribio la mauaji.
Mshukiwa wa kiume alikamatwa baadaye, kulingana na Geo TV ya Pakistani.
Waziri mkuu huyo wa zamani alionekana akipelekwa hospitalini huko Lahore. Msemaji wa chama alisema alikuwa amepigwa kwenye shin.
Afisa kutoka chama chake cha PTI, waziri wa afya wa mkoa Yasmeen Rashid, alisema Bw Khan yuko katika hali nzuri.
Polisi walitoa kanda ya video ya mtu waliyemkamata ambaye wanasema alijaribu kumuua waziri mkuu huyo wa zamani.
Haijulikani mahojiano yalifanyika chini ya hali gani lakini mtu huyo anaulizwa na polisi kwa nini alifyatua risasi, na anajibu: "Alikuwa akiwapotosha watu. Nilitaka kumuua. Nilijaribu kumuua."
Picha za video kutoka eneo la tukio zinaonyesha Bw Khan na wafuasi wake wakiwa wamepanda juu ya kontena kabla ya milio ya risasi kusikika.
Kisha Bw Khan anaonekana akipiga bata, huku wale walio karibu naye wakijaribu kumfunika.
Video nyingine inamuonyesha Bw Khan aliyekuwa na fahamu akiwa na bendeji kwenye mguu wake wa kulia akitolewa kwenye gari baada ya kupigwa risasi.
Mwanachama wa PTI pia anaonekana akiwa na kitambaa usoni na damu kwenye nguo yake, akisema kwamba watu wanapaswa kumwombea Bw Khan.
Waziri Mkuu wa sasa Shehbaz Sharif alilaani shambulizi hilo na kuamuru uchunguzi wa haraka ufanyike.
Mwezi uliopita, tume ya uchaguzi ya Pakistani ilimnyima Bw Khan kushikilia wadhifa wa umma katika kesi iliyoelezwa na mchezaji huyo nyota wa zamani kuwa ilichochewa kisiasa.
Alikuwa ameshutumiwa kwa kutangaza kimakosa maelezo ya zawadi kutoka kwa wakuu wa kigeni na mapato kutokana na madai ya mauzo yao. Zawadi hizo ni pamoja na saa za Rolex, pete na viunganishi vya mikono ya shati.
Pakistan ina historia ndefu ya vurugu mbaya za kisiasa. Katika tukio lililogonga vichwa vya habari duniani, Waziri Mkuu wa zamani Benazir Bhutto aliuawa katika mkutano wa hadhara mwaka 2007.
0 Comments