F Uvamizi wa wakulima na wafugaji ndani ya misitu ya hifadhi na mapori ya akiba ni chanzo cha vurugu za tembo. | Muungwana BLOG

Uvamizi wa wakulima na wafugaji ndani ya misitu ya hifadhi na mapori ya akiba ni chanzo cha vurugu za tembo.

 


Uvamizi wa wakulima na wafugaji ndani ya hifadhi ya hifadhi na mapori ya akiba ni chanzo cha vurugu za tembo. ¥ Na Ahmad Mmow, Lindi. ¥ Kitendo cha baadhi ya wafugaji na wakulima kuingia ndani ya hifadhi ya hifadhi na mapori ya akiba kimetajwa kuwa miongoni mwasababu zilizosababisha tembo kuingia katika makazi ya watu. ¥ Hayo yalielezwa jana na naibu katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii, Juma Mkomi katika kijiji cha Kibutuka, wilaya ya Liwale mkoa wa Lindi wakati wa zoezi la kuwaondoa tembo karibu na makazi ya watu na kuwavesha vifaa vitakavyotumika mienendo yao (kola/ GPS). 


¥ Mkomi ambae hayo baada ya kuzunguka kwa kuangalia hali ilivyo katika hifadhi ya hifadhi na mapori ya akiba alisema maeneo ya misitu ya hifadhi na mapori ya akiba yameharibiwa kwakiasi kikubwa na wakulima na wafugaji ambao wameingia ndani ya maeneo hayo nakufanya shughuli zao. Hali ambayo imechangia sababu zilizosababisha wanyama hao kuingia katika makazi ya watu. ¥ Mkomi alisema ndani ya hifadhi ya hifadhi na mapori ya akiba kuna mifugo mingi, vibanda vya makazi na mashamba. Kitendo ambacho kimesababisha zoezi lililokusudiwa kutumia muda mrefu tofauti na ilivyotarajiwa.



¥ " Wanafukuzwa lakini katika baadhi ya maeneo wanashindwa kupita kuna vibanda vya makazi na mashamba. Lakini pia kuna ng'ombe wengi," Mkomi alisema kwa masikitiko. ¥ Naibu katibu mkuu huyo alisema dhamira ya serikali kupitia wizara hiyo ni kumaliza changamoto hiyo. Hatahivyo aliweka wazi kwamba ili kufanikiwa azima hiyo kunahitajika ushirikiano na jitihada za pamoja baina ya wizara hiyo, wizara ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na wizara ya mifugo na uvuvi. Kwani kila wizara inaeneo la kushughulikia ikiwamo suala la mifugo na mipaka na mpango wa matumizi bora ya ardhi.




¥ Mtendaji huyo wa wizara ya maliasili na utalii aliwataka wananchi wanaoishi katika maeneo yanayotekelezwa zoezi hilo watoe ushirikiano, wasiwe kikwazo na wasiende wala kuingia na kufanya kazi za kibinadamu katika maeneo ambayo tembo hao wanapelekwa. ¥ Alisema lengo la zoezi hilo nikuhakikisha wanyama na binadamu wanaishi kwa usalama katika maeneo yao. Kwahiyo wananchi wasingie wala kuishi kwenye hifadhi na ushoroba. ¥ Alisema makundi ya wafugaji yamekwenda, yameingia na kuishi katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli za ufugaji wala kilimo. Kwahiyo viongozi wa wilaya,kata na vijiji wahakikishe wafugaji 




 na wakulima wanafanya shughuli zao katika maeneo yaliyotengwa kwa shughuli hizo. ¥ Mkomi aliwahakikishia wananchi kwamba wizara kupitia taasisi zilizo chini yake kwakutumia wataalamu na askari watakwenda kwawakati katika maeneo yatakayo ripotiwa kuwepo changamoto ya tembo na wanyapori wengine. ¥ Hatahivyo alitoa wito kwa serikali za wilaya ziwabaini nakuwachukulia hatua kali za kisheria viongozi na watendaji wanaowapitisha, kuwaingiza na kuwaruhusu wafugaji kuishi na kufanya shughuli ya ufugaji katika maeneo na vijiji visivyotengwa kwashughuli hiyo. Huku akibainisha wazi kuwepo viongozi na





watendaji wasio waaminifu kusababisha wafugaji kuvamia maeneo yasiyoruhusiwa kutumika kwa ufugaji. ¥ " Viongozi wa wilaya simamieni mpango wa matumizi bora ya ardhi. Wanyama wanavamia makazi ya watu, na watu wanavamia makazi ya wanyama. Kwahiyo viongozi hakikisheni wanakwenda katika maeneo rasimi yaliyotengwa," Mkomi alisisitiza. ¥ Kwaupande wake naibu kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama pori (TAWA), Mrage Kabange alisema mamlaka hiyo kwa upande wake imejipanga vema kumaliza changamoto hiyo. Lakini aliweka wazi kwamba ili kufanikiwa kunahitajika ushirikiano wa wananchi kwa taasisi hiyo na mamlaka





 nyingine. ¥ Kabange alitaja baadhi ya mipango iliyotekelezwa ili kufikia azima hiyo kuwa ni ujenzi wa nyumba maalumu 16 za kuishi askari wa wanyama pori katika baadhi ya vijiji ili waweze kufika haraka katika maeneo ya matukio. Ambapo katika mkoa wa Lindi nyumba hizo zimejengwa katika vijiji vya Ngumbu (Liwale), Nditi (Nachingwea) na Milola (Lindi) nyumba moja moja. ¥ Aliutaja mpango mwingine kuwa nimafunzo waliyopatiwa vijana 37 ambao watashirikiana na asikari wa wanyamapori. Pia imefanikiwa kupata pikipiki kwa ajili ya asikari, wakati pia kukiwa na mpango wa kuwapatia magari. Vifaa ambavyo vitatumika 






katika kufika haraka maeneo yenye changamoto. ¥ Nae mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, Dkt Eblate Mjingo alisema maeneo mengi yameharibiwa na mashamba na idadi ya tembo waliopo jirani na makazi ya watu ni kubwa. ¥ Dkt Mjingo alifuta dhana na fikra kwamba tembo wanaingia katika makazi ya watu kwasababu ya ukame na uhaba wa chakula. Alisema katika hifadhi kuna vyakula na maji ya kutosha bali tatizo ni wananchi kuingia katika maeneo ya misitu ya hifadhi na mapori ya akiba. Hali iliyosababisha tembo waende nakuingia kwenye makazi ya watu. ¥ Alisema kinachotokea sasa ni matokeo 




 ya uvamizi  katika maeneo hayo kwa muda mrefu. Ndipo tembo walianza kuhama nakusogea taratibu katika makazi ya watu na kukuta mazao ambayo kwao ni vyakula vitamu. Ikiwamo mabibo. Kwahiyo inakuwa vigumu kurudi kwa hiyari walikotoka ambako pia kumejaa ng'ombe, vibanda na mashamba. ¥ MWISHO ¥



Post a Comment

0 Comments