Madiwani Nachingwea wapitisha bajeti ya shilingi 37.00 bilioni.


Na Ahmad Mmow, Lindi. 

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi, jana liliridhia na kupitisha mapendekezo ya mpango na bajeti ya halmashauri hiyo wenye jumla ya shilingi 37,002,967,500.00 kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024. 


Akisoma mapendekezo ya mpango na bajeti katika kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Hajayanda Adon alisema halmashauri hiyo ya wilaya ya Nachingwea inatarajia kukusanya na kutumia shilingi 37,002,967,500 Kutoka katika vyanzo mbali mbali vya mapato. 


Adon alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni mapato ya ndani ya halmashauri hiyo, ruzuku toka serikali kuu, miradi ya maendeleo, ruzuku ya mishahara na mapato yanayotokanana huduma za afya. Ambapo mapato toka vyanzo vya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 yanatarajiwa kuwa shilingi 5,195,526,500.00. 


" Ambapo  shilingi 2,792,052,500.00 ni mapato yasiyofungwa, na shilingi 2,403,474,000 ni mapato fungwa. Bado halmashauri inaendelea kutafuta fedha kutoka  maeneo mbali mbali na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuongeza ukomo uliopo ili kutoa huduma kwa jamii kama ilivyo lengo kuu kwa halmashauri," alisema Adon.  


Alisema katika utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2021/2022 halmashuri hiyo ilikadiria kupoke mapato ya jumla ya shilingi 32,830,273,876.98 kutokana na mapato ya ndani, ruzuku ya mishahara, matumizi mengineyo na ruzuku ya miradi ya maendeleo. Ambapo hadi kufikia mwezi Juni, tarehe 30, mwaka 2022 halmashauri hiyo ilipokea jumla ya shilingi 28,377,817,737.30 ambazo ni sawa na asilimia 90 ya fedha zilizoidhinishwa. 


Kaimu mkurugenzi mtendaji huyo alisema kwa upande wa matumizi hadi kufikia tarehe 30, mwezi Juni, mwaka 2022 halmashauri hiyoilitumia jumla ya shilingi 26,535,422,088.01 ya mapato ya shilingi 28,377,817,737.30 yaliyo kusanywa. Ambayo ni sawa na asilimia 94 ya fedha zilizokuwa zimepokelewa. 


" Katika utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka 2022/2023 halmashauri ilikadiria kupokea mapato ya jumla ya shilingi 36,797,939,000 kutokana na mapato ya ndani, ruzuku ya mishahara, matumizi mengineyo na mirami ya maendeleo. Hadi kufikia Disemba 31, 2022 halmashauri ilipokea jumla ya shilingi 19,139,538,003.39 ambazo ni sawa na asilimi 50.22 ya fedha zilizoidhinishwa," alibainisha Adon. 


Aidha kaimu mkurugenzi mtendaji huyo aliweka wazi kwamba kwa upande wa matumizi hadi kufikia tarehe 31, mwezi Disemba, mwaka 2022 ilikuwa imetumia jumla ya shilingi 15,395,555,850.17 ya mapato ya shilingi 19,139,538,003.99. 


Kikao hicho maalumu cha baraza la madiwani wa wilaya ya Nachingwea kilitanguliwa na kikao cha kawaida robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Post a Comment

0 Comments