https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mamia wajitokeza kumzika mwandishi wa habari wa Rwanda | Muungwana BLOG

Mamia wajitokeza kumzika mwandishi wa habari wa Rwanda


 Mamia ya watu walishiriki katika mazishi ya mwandishi wa habari John William aliyefariki katika ajali ya gari, huku mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yakitaka uchunguzi huru kuhusu kifo chake.


Wanahabari wengi nchini humo, marafiki, na wanafamilia walishiriki katika mazishi haya siku ya Jumapili, huku kukiwa hakuna mengi yaliyosemwa kuhusu kazi ya marehemu au jinsi kifo chake kilivyotokea.


Frank Habineza kutoka chama cha upinzani cha Democratic Green Party of Rwanda, Victoire Ingabire na Bernard Ntaganda ni miongoni mwa wanasiasa waliohudhuria mazishi hayo.


"Hatutasahau mchango wako wa thamani katika kukuza uhuru wa vyombo vya habari katika mazingira yenye changamoto", Bi Ingabire alisema kuhusu kifo cha Bw Ntwali.


Polisi walisema Bw Ntwali alifariki papo hapo kwenye ajali ya barabarani siku ya Jumanne usiku wakati bodaboda aliyokuwa amepanda ilipogongwa na gari, dereva akakamatwa, polisi waliongeza.


Lakini Human Rights Watch ilisema kwamba "kuna sababu nyingi za kutilia shaka" maelezo ya polisi na kutaka "utaalamu wa kimataifa kubaini kama aliuawa au la."

Post a Comment

0 Comments