Mlipuko wa msikiti wa Pakistan: Polisi walilengwa katika shambulio la kujitoa muhanga lililoua watu 59

 


Takriban watu 59 wameuawa na shambulio la bomu la kujitoa mhanga ambalo linaonekana kuwalenga polisi waliokuwa wakisali katika msikiti mmoja huko Peshawar, Pakistan.


Msikiti huo uko ndani ya eneo la makao makuu ya polisi yenye ulinzi mkali.


"Magaidi wanataka kujenga hofu kwa kuwalenga wale wanaotekeleza jukumu la kuilinda Pakistan," Waziri Mkuu Shehbaz Sharif alisema.


Kundi la Taliban la Pakistan lilikana kuhusika baada ya madai ya awali ya mmoja wa makamanda wake.


Kundi hilo lilimaliza usitishaji mapigano mwezi Novemba, na ghasia zimekuwa zikiongezeka tangu wakati huo.


Mnamo Disemba ililenga kituo cha polisi - kama Peshawar,kaskazini-magharibi mwa nchi- na kusababisha vifo vya wanamgambo 33.


Msemaji wa hospitali aliambia BBC kwamba idadi ya waliofariki ilifikia 59, huku watu 157 wakiwa wamejeruhiwa.


Kati ya maafisa wa polisi 300 na 400 walikuwa katika eneo hilo wakati huo, mkuu wa polisi wa Peshawar Muhammad Ijaz Khan aliambia vyombo vya habari vya ndani.

Post a Comment

0 Comments