https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mwanamke wa kwanza wa Palestina atawazwa kuwa mchungaji katika kanisa la Kilutheri huko Jerusalem | Muungwana BLOG

Mwanamke wa kwanza wa Palestina atawazwa kuwa mchungaji katika kanisa la Kilutheri huko Jerusalem

 


Katika maeneo mengi ya kikristo duniani, kuwa na viongozi wa kike wa kanisani si jambo geni tena. Lakini mpaka sasa, Nchi Takatifu - ambapo matukio mengi katika Biblia yamewekwa - ilikuwa haijawahi kutokea mwanamke kutoka ndani ya nchi hiyo kuwa kiongozi wa dini.


Siku ya Jumapili,ilikuwa sherehe ya raia wa Palestina kutoka Jerusalem, Sally Azar, kuwa mchungaji mwanamke wa kwanza katika kanisa la Kilutheri katikati ya Mji Mkongwe, iliyohudhuriwa na mamia ya watu kutoka mataifa mbalimbali.


"Nilifurahishwa zaidi kuona msisimko wa watu wengine," Mchungaji Azar alisema. "Ni hisia isiyoelezeka kuchukua hatua hii kwa kuungwa mkono na kanisa."


"Nina matumaini kwamba wasichana na wanawake wengi watajua kuwa jambo hili linawezekana na hata wanawake wengine kutoka kwenye makanisa mengine watajiunga nasi. Najua itachukua muda mrefu, lakini nadhani itafurahisha zaidi ikiwa hii hali itabadilika nchini Palestina.


" Wakristo ni wachache katika maeneo ya Palestina, Israel na Jordan. Wakristo wengi hapa ni wa Kanisa la Orthodox la Ugiriki na kuna Makanisa ya kikatoliki ya Latini, ambayo hayaruhusu mapadre wanawake.


Hata hivyo, idadi ya wanawake wanaowekwa wakfu katika Makanisa ya Kiprotestanti inaongezeka katika miongo michache iliyopita. Na hii inawapa fursa ya kuwa viongozi wa shule na hospitali katika ardhi takatifu.

Post a Comment

0 Comments