Mwili uliozikwa na "moyo wa dhahabu" miaka 2,300 iliyopita huko Misri

 


Tutankhamun amekuja na mshindani. Huyu ni kijana mwingine aliyekuwa wa tabaka la juu la Misri ya kale na ambaye alitiwa moyo wa dhahabu miaka 2,300 iliyopita.


Mwili wa kijana huyo, ambaye inakadiriwa kuwa alikufa kati ya umri wa miaka 14 na 15, ulipatikana mwaka wa 1916. Hata hivyo, mabaki yalibaki kuhifadhiwa kwa zaidi ya karne, pamoja na kadhaa zaidi, katika maghala ya Makumbusho ya Misri huko Cairo, bila kuchunguzwa kwa kina na wataalam.


Hata hivyo, hii ilibadilika wakati timu iliyoongozwa na Dk. Sahar Saleem, kutoka Chuo Kikuu cha Cairo, iliamua kuangalia mwili huu, kwa kutumia CT scanner.


Picha zilizopatikana zilifichua kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na hirizi 49 za aina 21 tofauti, nyingi zikiwa za dhahabu na, kwa sababu hiyo, mwili huo  umebewa jina "mvulana wa dhahabu", Saleem alitangaza katika nakala iliyochapishwa katika Medicinejournal .


Hazina iliyofichwa

Uchunguzi huo ulifanya iwezekane kubaini kwamba kijana huyo alikuwa wa tabaka la juu, kwa kuwa "alikuwa na meno na mifupa yenye afya, bila ushahidi wa utapiamlo au ugonjwa" na kwa sababu mabaki yake yaliwekwa chini ya mchakato "wa hali ya juu" wa kukamua, ambayo ni pamoja na kuondolewa kwa ubongo na viscera".


Picha hizo zilionyesha kuwa chini ya sanda zilizoufunika mwili wa kijana huyo kulikuwa na kitu cha urefu waa vidole viwili karibu na uume wa marehemu ambao haujatahiriwa, ulimi wa dhahabu mdomoni na moyo wenye umbo la mende pia uliotengenezwa kwa nyenzo hiyo ya thamanivambayo ilikuwa chini ya ya  kifua.


Saleem alikumbuka kwamba Wamisri wa kale waliweka hirizi juu ya maiti za marehemu wao kwa madhumuni ya "kuwalinda na kuwapa nguvu" katika maisha ya baada ya kifo. "Ulimi wa dhahabu ndani ya kinywa ulitaka kuhakikisha kwamba marehemu anaweza kuzungumza katika maisha ya baadaye," alieleza mtaalamu huyo.


Picha hizo pia zilionyesha kuwa mwili wa kijana huyo ulikuwa umevaa viatu na taji za maua ya feri.


Mwili huo  ambao unakadiriwa kutoka (c. 332-30 BC), ulipatikana kusini mwa nchi, mwaka  1916; Miaka sita kabla ya msafara ulioongozwa na Mwingereza Howard Carter ulipata kaburi la Tutankhamun kwenye Bonde la Wafalme.


Nje kulikuwa na maandishi kwa Kigiriki na ndani yalifanywa kwa mbao. Maiti ilikuwa na kinyago cha dhahabu kichwani.


Misri ilishuhudia uchimbaji mkubwa katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20 ambao ulisababisha kufukuliwa kwa maelfu ya miili ya zamani iliyohifadhiwa, mingi ikiwa imefungwa na ndani ya majeneza yao," alisema.


"Tangu kufunguliwa kwake mnamo 1835, Jumba la Makumbusho la Misri huko Cairo limetumika kama ghala la vitu hivi vilivyopatikana na jumba la chini limejaa maiti nyingi ambazo zimefungiwa kwa miongo kadhaa bila kuchunguzwa au kuonyeshwa," aliongeza.


Hapo awali, bandeji ziliondolewa kwenye maiti na miili ilikatwa kwa uvamizi kwa madhumuni ya utafiti na burudani, msomi huyo alisema.


Lakini sasa, matumizi ya kompyuta inaweza kuwa chombo kikubwa cha kuchunguza mengi ya mabaki haya bila kuwadhuru, jambo ambalo litatuwezesha kuzama "zaidi kuhusu afya, imani na uwezo wa binadamu wa zamani," mtaalamu huyo alisema. . . .


"Kompyuta inawakilisha maendeleo makubwa katika radiolojia. Badala ya kutumia picha moja, mamia ya makadirio ya sehemu nyembamba (vipande) vya mwili vinaweza kuunganishwa ili kuunda mfano kamili wa pande tatu, "alihitimisha. 

Post a Comment

0 Comments