Nyaraka za siri zimepatikana katika nyumba ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence katika ugunduzi wa hivi karibuni wa karatasi za siri katika nyumba za maafisa ambao wamehudumu katika nyadhifa za juu serikalini.
Nyaraka hizo, zilizogunduliwa na wakili wa Bw Pence wiki iliyopita nyumbani kwake Indiana,na zimekabidhiwa kwa FBI.
Wachunguzi tayari wanachunguza umiliki wa nyaraka za Rais Joe Biden na Rais wa zamani Donald Trump.
Bw Trump anakabiliwa na uchunguzi wa makosa ya jinai kwa madai ya kumiliki karatasi vibaya.
Wawakilishi wa Bw Pence walituma barua katika maktaba ya hifadhi ya Kitaifa kuwaarifu kuhusu hati hizo.
FBI walifika nyumbani kwa makamu wa rais wa zamani kuchukua nyaraka hizo, bila kutumia "taratibu za kawaida" na kuomba karatasi hizo, wanasheria waliongeza katika barua nyingine tofauti.
Chini ya sheria ya rekodi za Rais, rekodi za Ikulu zinapaswa kwenda kwenye maktaba ya hifadhi ya Kitaifa mara tu usimamizi utakapomalizika.
Sheria inahitaji faili kama hizo kuhifadhiwa kwa usalama.
"Idadi ndogo ya hati zilizo na alama za siri" "ziliwekwa kwenye masanduku bila kukusudia na kusafirishwa" hadi nyumbani kwa Bw Pence mwishoni mwa urais wa Bw Trump, wakili wake aliandika katika barua iliyoshirikiwa na vyombo vya habari vya Marekani.
Matukio ya hivi karibuni yaliibuka baada ya Bw Pence kutafuta usaidizi wa kisheria kutoka kwa wataalamu katika kushughulikia hati za siri "kutokana na tahadhari nyingi"
