Singapore: Interpol inamtafuta mwanamke anayeendesha utapeli wa mitihani

 


Polisi imetoa tahadhari kuhusu mwanamke mmoja anayeendesha utapeli mkubwa wa katika mitihani nchini Singapore uliohusisha simu za mkononi na headphones wanavyowekewa wanafunzi.


Poh Yuan Nie, mwenye umri wa miaka 57, hushirikiana na watu wengine watatu ambao tayari, wamefungwa gerezani.


Poh, ambaye ni mkuu wa zamani wa shule katika kituo cha masomo ya ziada (tuition) , alikua anakaribia kuanza kutumikia kifungo cha miaka minnemwezi Septemba mwaka jana, lakini hakujisalimisha mwenyewe kama ilivyotarajiwa.


Anadhaniwa kuwa ametoroka Singapore.


Polisi katika mji wa jimbo walimetoa kibali kwa ajili ya kumkamata Bi Poh, ambaye pia anafahamika kama Pony, mwezi Novemba mwaja jana. Waliwasilisha ‘’taarifa ya hatari’’ kwapolisi ya kimataifa -Interpol, katika mwezi uliofuatia na wakatoa taarifa kwa yeyote anayefahamu mahala alipo kutoa taarifa.


Taarifa hiyo nyekundu inayataka mashirika ya usalama kumsaka na kumkamata mtukabla ya kumrejesha alikotendea kosa au kuchukua hatua sawa ya kisheria.


Wizi huo wa mitihani ulifanyika kwa siku kadhaa katika mwezi Oktoba 2016, wakati wa mithani mitatu ya kujiunga na vyuo vya mafunzo ya elimu ya juu.

Post a Comment

0 Comments