Ujerumani yafutilia mbali uwezekano wa kupeleka ndege za kivita Ukraine

 


Kansela wa Ujerumani amefutilia mbali uwezekano wa kutuma ndege za kivita nchini Ukraine, siku chache tu baada ya kujitolea kusambaza vifaru nchini humo.


Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani, Olaf Scholz alionya dhidi ya kuchochae vita kuputia silaha .


Lakini Ukraine imeomba mataifa washirika kuunda "muungano wa ndege za kivita" ili kuimarisha uwezo wao.


Marekani ilisema itajadili wazo la kusambaza ndege "kwa uangalifu mkubwa" na Kyiv siku ya Alhamisi.


Katika mahojiano na Tagesspiegel, Bw Scholz alisema lengo lake lilikuwa utoaji wa vifari vya Leopard 2 vilivyotengenezwa Ujerumani.


"Ukweli ndio tu tumefanya uamuzi [juu ya kutuma vifaru] na mjadala unaofuata unaanza nchini Ujerumani, hiyo inaonekana kuwa ya kipuuzi", alisema.


Siku ya Jumatano Ujerumani iliazimia kusambaza vifaru 14 vya Leopard 2 kwa Ukraine, baada ya wiki za shinikizo kutoka kwa washirika.


Kufuatia kujitolea kwa Ujerumani kutuma vifaru hivyo , Marekani ilisema kuwa itaipatia Ukraine vifaru vyake vya M1 Abrams.


Naibu waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Andrii Melnyk, ametoa wito wa kuundwa kwa "muungano wa ndege za kivita" utakaoipatia Ukraine ndege za Marekani F-16s na F-35, Eurofighters, Tornados, Rafales za Ufaransa na ndege za Gripen za Uswidi.


Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak aliuambia Mtandao wa Televisheni ya Uhuru wa Ukraine pia wanahitaji makombora "kupunguza kwa kiasi kikubwa silaha muhimu ya jeshi la Urusi".


Naye rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliunga mkono hilo katika hotuba yake ya kila siku ya video ambapo alisema nchi hiyo inahitaji kombora la ATACMS lililotengenezwa na Marekani, ambalo lina uwezo wa kusafiri umbali wa maili 185 (297km).

Post a Comment

0 Comments