Ujio wa Aucho wamfurahisha kocha Nabi

 


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Mohammed Nabi, amekiri kufurahishwa na hatua ya mazoezi ya mazoezi kwa Kiungo kutoka nchini Uganda Khalid Aucho.


Kwa siku kadhaa Aucho amekuwa nje ya kikosi cha Young Africans, ambacho kinaendelea na harakati za kutetea mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara 'ASFC'.


Kocha Nabi amesema, kiungo huyo tangu Jumamosi amekua akifanya mazoezi binafsi baada ya kupona majeraha yake, na anaamini kurejea mazoezini kutaongeza changamoto kwa wengine wa Young Africans.


“Nimefurahi kuona kikosi changu kikiwa imara kutokana na uwepo wa baadhi ya wasanii ambao walikosekana katika michezo kwa ajili ya majeraha.”


“Kati ya hao ni Aucho ambaye amepona majeraha yake yaliyomsababisha aikose michezo.”amesema kocha Nabi.


Aucho a mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari wa Klabu ya Young Africans, ambao wanachukua tahadhari ili kiungo huyo asijitoneshe majeraha kumuweka nje kwa muda wa siku kadhaa.

Post a Comment

0 Comments