Urusi yazuia upatikaji wa taarifa kutoka kwenye tovuti za CIA na FBI

 


Urusi imefunga wavuti wa mashirika ya upelelezi ya Marekani ya CIA , FBI moja na ule wa Wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani. Hatua hiyo iliyotekelezwa Ijumaa imefuatia ombi la taasisi ya usimamizi wa mawasiliano ya kiteknolojia-Roskomnadzor.


Tovuti hizi hutumiwa na Marekani kutoa taarifa kuhusu vitisho dhidi ya usalama wa taifa hilo.


Zimefungwa tangu Januari 26, huduma ya mawasiliano ya Urusi Roskomnadzor imeiambia BBC kwamba "Tovuti hizi zina taarifa zisizo na maana kijami" zilipatikana katika vyanzo hivyo, pamoja na udhalilishaji wa jeshi la Urusi.


Kulingana na Roskomnadzor, tovuti hizo "ni za mfumo wa taifa unaosababisha uhasama kwa nchi" kwa kutoa taarifa zenye lengo la kuyumbisha hali ya kisiasa na na kijamii kwa lugha ya Kirusi.


Mwezi Mei mwaka jana, Mkuu wa tume ya usalama ya bunge la Urusi (Duma) alisema machapisho ya CIA nchini Urusi yanachochea uhaini.


Tarehe 2 Mei, CIA iliweka mtandaoni videokwa lugha ya kirusi katikachaneli yake ya YouTube , ambayo ilisshauri juu watu wanavyoweza kuwasiliana nao kwa usalama na kuwafikishia taarifa za ujasusi.


Katika kujibu hatua hiyo, Idara ya huduma za ujasusi wa kigeni ya Urusi ilifungua wavuti wa siri mwezi Aprili, ambapo huwataka watu kuishirikisha taarifa "vitisho kwa usalama wa Shirikisho la Urusi."


Mapema mwezi Januari, ofisi ya mwendesha mashita mkuu wa jeshi wa jimbo la Vladimir pia aliwasilisha ombi la kisheria la kuzuiwa kwa wavuti wa habari za Umoja wa Mataifa (UN news) nchini Urusi, lakini Ijumaa alikanusha mwenyewe madai hayo. Mahakama ilipuuzilia mbali kesi ya ombi hilo.

Post a Comment

0 Comments