VIDEO: Watu 48 wakamatwa, Polisi watoa onyo


Jeshi la Polisi Nchini kupitia kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU) katika operesheni mbalimbali wamefanikiwa kukamata jumla ya mifugo 2,225 ambayo ilikua inasafirishwa bila kufuata utaratibu na iliyoingizwa katika mapori tengefu pamoja na vyanzo vya maji.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema katika operesheni hiyo iliyofanyika mwezi huu watuhumiwa 48 walikamatwa wakiwa na mifugo hiyo kwa makosa mbalimbali.

Kamanda Pasua amesema makosa hayo ni pamoja na kuingiza mifugo katika vyanzo vya maji, kusafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine bila kuwa na kibali na kuingiza mifugo kiholela katika mapori tengefu ama vyanzo vya maji.

ACP Pasua alibainisha kati ya mifugo iliyokamatwa 1,263 ilikamatwa katika pori tengefu la Pololeti wilayani Ngorongoro na 962 ilikamatwa ikisafirishwa kutoka Mkoa wa Morogoro kwenda mkoa wa Ruvuma bila ya kufuata taratibu za kisheria.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI........USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Post a Comment

0 Comments